Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maua Sama, AliKiba kunani?

Dodoma Pict

Muktasari:

  • Juzi kwenye Mkutano wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika jijini Dodoma wakali hao waliongozana huku wakiwa wameshikana mikono jambo ambalo lilitafsiriwa kuwa huenda wakawa na ukaribu mwingine nje ya kazi.

UKARIBU wa Maua Sama na Alikiba haujawahi kufafanuliwa hadharani, lakini wote ni wanamuziki wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya Bongo Fleva.

Juzi kwenye Mkutano wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika jijini Dodoma wakali hao waliongozana huku wakiwa wameshikana mikono jambo ambalo lilitafsiriwa kuwa huenda wakawa na ukaribu mwingine nje ya kazi.

Mara kadhaa Maua amekuwa akiposti kuwa anampenda Kiba, kauli ambazo zimekuwa zikiwachanganya mashabiki kama huenda wawili hao wakawa wapo penzini.

Hata akifanya mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari Sama amekuwa akiongea kuwa anampenda Kiba.

Wote wawili, hata hivyo, hawajaweka wazi kama kila mmoja keshaingia katika uhusiano mpya kwani tangu Ali Kiba aachane na mke wake wa zamani, Mkenya Amina Khalef mwaka 2023 hadi sasa hajahusishwa na mrembo yeyote.

Vivyo hivyo kwa Maua ambaye amekuwa akiweka maisha yake ya uhusiano kiusiri jambo ambalo limekuwa na ugumu kwa baadhi ya mashabiki kujua nani anammiliki mrembo huyo, japo siku za nyuma aliwahi kuhusishwa na 'mzungu' ambaye hakutajwa jina akidaiwa kuwa ndiye aliyemnunulia gari aina Toyota Rav4 ya mwaka 2017 alilokuwa akitembelea kimwana huyo.

Mrembo huyo alikuwa akisema 'No comment' katika maswali kuhusu bei ya gari hiyo, au kuhusu kama alinunuliwa au alinunua mwenyewe.

Dom 01

Mbali na hilo pia huenda wakawa wanafanya hivyo ili kuwapa umakini mashabiki tu ili endapo watatoa ngoma nyingine iweze kufuatiliwa na wengi.

Sasa hapo kwenye kushirikiana kuna kolabo nyingine zikitokea huwa zinaacha maswali mengi.

Maua Sama na Alikiba wamekuwa na ushirikiano wa karibu katika kazi zao za muziki na wamefanya kazi pamoja katika nyimbo mbili, "Nioneshe" na "Itakuwaje" iliyotoka mwaka 2024.

Ushirikiano huu umeonyesha muunganiko mzuri wa kikazi kati yao, na kila walipoingia studio pamoja wameweza kutoa nyimbo zilizopokewa vyema na mashabiki.

Maswali ni je kuna nini kinaendelea baina ya nyota wao wawili wa muziki wa Afrika?


KOMBINESHENI YAO

Waimbaji hao wanaendelea kufanya vizuri na wimbo wao mpya, Itakuwaje (2024) ambao tunaweza kusema unathibitisha kuwa kuna kitu kinaendelea upande wa kazi baina ya wawili hao.

Huu ni wimbo wa pili kwa Alikiba kushirikishwa na msanii wa kike kwa mwaka jana baada ya ule wa Nandy, Dah! (2024), huku The African Princess huyo akisikika pia katika EP ya kwanza ya Kiba, Starter (2024).

Ikumbukwe Maua Sama alitoka kimuziki baada ya kuachia wimbo wake, So Crazy (2013) akiwa na Mwana FA ila awali aliwatumia wimbo huo wasanii kadhaa akiwamo Alikiba, Ommy Dimpoz na Ben Pol ili washiriki lakini haikuwezekana.

Dom 01 (1)


Tangu ametoka kimuziki zaidi ya miaka 10 iliyopita Maua Sama hajatoa albamu ila ameachia EP mbili, Cinema (2022) na Sama (2024), na katika EP zote Alikiba ameshirikishwa na ndio maana tunasema kuna kitu kati yao.

Katika EP ya kwanza, Cinema (2022), Alikiba kutokea Kings Music alisikika katika wimbo 'Nioneshe' ambao ulifanya vizuri, na katika EP hii ya pili, Sama (2024), Kiba kashirikishwa katika wimbo huo 'Itakuwaje' ambao video yake imetoka wiki hii.

Ni wazi Maua amegundua ana muunganiko mzuri wa kikazi na Alikiba, kila wakiingia studio wanatoa kitu kizuri kinachowafaa mashabiki wake, sasa kwanini kazi isifanyike kama ni hivyo?

Na katika EP hii ya pili, Sama (2024), Maua pia amemshirikisha Nandy, huyu ni msanii mwingine wa kike Bongo ambaye anamuelewa sana Alikiba linapokuja suala la kazi, tayari amempa shavu katika nyimbo mbili, Nibakishie (2020) na Dah! (2024).

Kombinesheni ya wawili hao imekuwa ikifanya vizuri na kutokana na sauti nzuri wanazoimba zikiwapagawisha mashabiki wao.

Kati ya maswali ni je, Kiba anataka kumsaini Maua, ambaye ameibuliwa MwanaFA, katika lebo yake ya Kings Music? Muda utaongea.