Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa 10 wa kiume matajiri Nollywood 2015

Richard Mofe Damijo

Muktasari:

Walio wengi wametumia nafasi hiyo kutengeneza mkwanja. Leo katika safu hii tunakuletea mastaa 10 wa kiume ambao ni matajiri Nollywood, ambao wametengeneza mkwanja kupitia uigizaji.

HAKUNA ubishi tasnia ya uigizaji ya Nollywood imetengeneza fursa nyingi za utafutaji wa mkwanja kwa mastaa wa kike na kiume.

Walio wengi wametumia nafasi hiyo kutengeneza mkwanja. Leo katika safu hii tunakuletea mastaa 10 wa kiume ambao ni matajiri Nollywood, ambao wametengeneza mkwanja kupitia uigizaji.

1. Richard Mofe Damijo

Kitaaluma ni Mwandishi wa Habari na mchapishaji wa Jarida la Richard Eyimofe Mofe-Damijo linalojulikana kwa kifupi RDM.

Ameshika nafasi ya kwanza katika orodha ya mastaa matajiri Nollywood kwani anamiliki mkwanja mnono.

Richard ameonekana katika filamu nyingi, pia ameigiza filamu maarufu tangu mwishoni mwa miaka ya 1990. Mwaka 2005 alishinda tuzo ya African Movie Academy kipengele cha Mwingizaji Bora wa Kiume wa muda mrefu.

2. Jim Iyke

Jim Iyke (James Ikechukwu Esomugha) ni mwigizaji machachari. Umaarufu wake unatokana na uigizaji na anapendwa zaidi na warembo kutokana na ulegevu wa macho yake.

Pia Jim ni mwandishi wa nyimbo na mwimbaji. Kitu ambacho kimempa utajiri zaidi ni uigizaji wa filamu nyingi ambazo amekuwa akilipwa fedha nzuri, ameigiza zaidi ya filamu 150. Ameingiza fedha nyingi kupitia uigizaji, matangazo na biashara kadhaa anazomiliki.

3. Nkem Owoh (Osuofia)

Huyu jamaa ukimuona katika filamu anazoigiza unaweza kudhani ana upungufu wa akili. Ni kutokana na tabia yake ya ubishi, ukoloni na mengine mengi.

Nkem Owoh ni mchekeshaji na mwigizaji anayefahamika zaidi ya kwa jina la Osuofia, alianza uigizaji zamani kwani ni miongoni mwa waigizaji wa mwanzo Nollywood.

Mwaka 2003 aliigiza filamu ya Osuofia jijini London na tangu hapo ameendelea kuwa Mfalme wa wachekeshaji Nollywood kwani rekosdi ya mauzo ya filamu hiyo mpaka sasa haijavunjwa. Hilo pekee limetosha kumfanya jamaa huyu kuwa tajiri.

4. Chinedu Ikedieze (Aki)

Anafahamika zaidi Nollywood, kwa kimo chake na mambo yake katika uigizaji, wengi wanadhani ni mtoto.

Anamiliki mali nyingi na ni tajiri ukilinganisha na waigizaji wengine wa kiume Nollywood.

Chinedu Ikedieze amekuwa akichuana na mwigizaji mwenzake Osita Iheme ambaye amekuwa naye bega kwa bega katika kila filamu baada ya kufanya vizuri katika filamu ya Aki na Ukwa.

Mwaka 2007 Ikedieze alipata tuzo ya Lifetime Achievement katika tuzo za African Movie Academy.

5. Osita Iheme (Pawpaw)

Anachuana na Aki. Yeye amefanikiwa kutokana na mkwanja anaoutengeneza kulandana na ule wa Ikedieze.

Anajulikana zaidi kama Pawpaw katika filamu ya Aki na Ukwa, lakini naye pia alipata tuzo ya Lifetime Achievement mwaka 2007.

Kwa mwaka huu wa 2015 watu wengi wanaamini anastahili kupata tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kiume Nollywood kutokana na umahiri wake unaoendelea kukua siku baada ya siku.

Analipwa mkwanja mnono, lakini pia yeye mwenyewe amefanikiwa kuingiza fedha nyingi kupitia uigizaji.

6. Ramsey Nouah

‘My Love’ ni filamu ambayo ilimpa umaarufu mkubwa mwigizaji huyu na kufahamika zaidi kote duniani.

Ramsey Nouah ni kati ya waigizaji ambao wanaingiza fedha nyingi katika malipo kutokana na umaarufu, pia ukongwe katika uigizaji.

Ramsey alionekana katika filamu ya kwanza kutengenezwa katika tasnia ya uigizaji Nollywood inayojulikana kwa jina la Silent Night.

Filamu nyingine alizoigiza ni pamoja na Battle Of Love, When Love Dies, Dangerous Twins, To Love an Angel, A Private Storm na The Figurine.

Nouah anaingiza fedha nyingi kupitia mirabaha, lakini pia biashara zake mbalimbali anazozifanya nchini Nigeria.

7. Desmond Elliot

Desmond Elliot ambaye pia ameingia katika orodha ya mastaa matajiri kwa mwaka 2015 alijulikana zaidi kupitia filamu za Painful World 2 (2006), Unfinished Business 2 (2007) na True Colors 2 (2008).

Ameigiza katika zaidi ya filamu 200. Ameigizaji mkwanja mnono ambao ameuwekeza katika miradi mbalimbali, fedha hizo aliingiza kupitia uigizaji na matangazo.

8. Mike Ezuruonye

Wengi wanadhani huyu jamaa ni Mghana, lakini wapo wanaoamini kwamba amekuwa akiigiza katika filamu chache ukilinganisha na waigizaji wengine.

Ukweli ni kwamba Mike Ezuruonye alianza uigizaji kitambo na ni miongoni mwa waigizaji kivutio mbele ya macho ya mashabiki.

Amekuwa akifanya vizuri na kuliteka soko kila anapoingizwa katika filamu yoyote na ndiyo maana analipwa fedha nzuri.

9. Nonso Diobi

Mwigizaji Nonso Diobi ambaye alionekana kwa mara ya kwanza katika filamu ya ‘Border Line’ amejulikana zaidi kupitia filamu ya ‘Hatred’.

Ameigiza katika filamu maarufu zaidi ya 60 na ni balozi wa kampuni moja kubwa ya simu nchini Nigeria.

Anamiliki biashara kadhaa na amefanikiwa kuingiza mkwanja mnono kupitia uigizaji, lakini pia matangazo ya biashara.

10. John Okafor (Mr Ibu)

Huyu jamaa kwa jinsi anavyoigiza, unaweza kukasirika lakini huwezi kuacha kuendelea kuitazama filamu yake.

John Okafor wengi wanamtambua kama Mr. Ibu, hana akili anapokuwa anapiga mzigo, lakini kazi hiyo hiyo inamfanya amiliki mkwanja mnono.

Mbali na kuigiza, Mr. Ibu anatengeneza fedha kupitia umiliki wa klabu ya mpira na ni miongoni mwa waigizaji wa kiume ambao ni matajiri Nollywood.