Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Masha Love atoa neno ndoa na Mose Iyobo

MASHA Pict

Muktasari:

  • Pia alisema kwa sasa anataka kuolewa na Mose ili kuondoa nuksi, kwani kukaa bila ndoa kwao haileti picha nzuri.

MWANADADA mwenye mvuto wa aina yake Bongo, Masha Love amefichua ukweli juu ya kuridhia ndoa na dansa wa Diamond, Mose Iyobo na ameamua kuolewa ili kutoa nuksi.

Masha Love ambaye hujulikana sana mtandaoni kwa video zake za kuchezesha matiti, aliliambia Mwanaspoti kitu cha kwanza kukubali kwake kutaka kuolewa na Mose Iyobo ni mapenzi ya muda mrefu aliokuwa nao kwa dansa huyo, pia ameona ni mabadiliko kwake kwani kabla ya kuwa naye alishawahi kuwa kwenye mahusiano na hakuweza kudumu muda mrefu.

Pia alisema kwa sasa anataka kuolewa na Mose ili kuondoa nuksi, kwani kukaa bila ndoa kwao haileti picha nzuri.

“Kitu kikubwa watu ambacho hawakijui kwa sasa nataka kuolewa kutoa nuksi, si unajua mwanamke kukaa bila ndoa haileti picha nzuri na uzuri tumeshaanza maandalizi madogo madogo ya ndoa, hivyo jambo likiwa tayari tutaweka wazi tu," alisema Masha Love.

Masha Love na Mose Iyobo wapo katika mahaba mazito kwa muda mrefu, tangu dansa huyo alipotemana na mama mtoto wake, Aunty Ezekiel na inadaiwa wapo katika harakati za kuoana.