Marioo aliamsha kweli

Sunday September 19 2021
marioo pic 1

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Marioo ameliamsha kweli katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Msanii huyo aliingia na pikipiki iliyokuwa na matairi manne huku akisindikizwa na wenzake wanne waliokuwa na pikipiki za matairi mawili.

marioo pic

Balaa kubwa walilionyesha hao wanne ambao walimsindikiza Marioo katika pikipiki kwani walikuwa wanafanya michezo mbalimbali.

Walikuwa wanatembea na tairi moja, wanasimama wakiwa na pikipiki pamoja na mambo mengine kibao.

Wakati huo hao wanne wakiendelea kuonyesha kichezo hiyo Marioo aliendelea kutumbuiza jukwaani huku baadhi ya mashabiki wakimfuatisha pamoja na wengine kucheza.

Advertisement

Nyimbo ambayo aliwavutia wengi waliokuwa Uwanjani hapo ni ile ya ‘Bia tamu’.

Mara baada ya kumaliza hapo alibebwa katika pikipiki na kuondoka hapo uwanjani.

Advertisement