Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Marco wa Zabron Singers alivyopambania uhai kwa siku 10

Muktasari:

  • Mjomba wa marehemu Emanuel Zabron leo Agosti 22, 2024 ameliambia Mwananchi kuwa  tatizo hilo lilitokea ghafla Jumapili Agosti 11,2024, akiwa nchini Kenya alipokwenda kwa ajili ya huduma yake ya uimbaji

 Familia ya alikuwa mwimbaji wa kundi la Zabron Singers Marco Joseph imesema chanzo cha kifo cha ndugu yao ni tatizo la moyo lilitokea ghafla akiwa nchini Kenya.

Mjomba wa marehemu Emanuel Zabron leo Agosti 22, 2024 ameliambia Mwananchi kuwa  tatizo hilo lilitokea ghafla Jumapili Agosti 11,2024, akiwa nchini Kenya alipokwenda kwa ajili ya huduma yake ya uimbaji.

“Tatizo hili lilitokea ghafla sana wakati anaendesha gari na ndipo alipaki na kuita wenzake,” amesema.

Ameeleza baada ya tatizo hilo hakuweza kuendelea na huduma ilibidi arudi Mwanza na Ijumaa tarehe 16 alienda kufanyiwa vipimo katika Hospitali ya Bugando ndipo majibu yalionesha anashimo kubwa kwenye moyo ambalo ndilo lililopelekea mshtuko huo akiwa nchini Kenya.

“Baada ya majibu hayo ilibidi aje siku hiyo ya Ijumaa jioni na kwenda moja kwa moja Taasisi ya Jakaya Kikwete kwa vipimo zaidi, tulivyofika vipimo vilikuwa changamoto kwa sababu ilikuwa wikiendi ilibidi turudi hospitali siku ya Jumatatu ili kupata huduma.

"Baada ya vipimo kufanyika alipangiwa siku ya Jumatano kwa ajili ya upasuaji. Baada ya upasuaji madaktari walituita wakasema mgonjwa anatokwa damu nyingi baada ya kuwekewa kifaa maalumu cha kusaidia katika upumuaji,"amesema ndugu huyo wa marehemu
Hata hivyo, amesema awali marehemu hakuwahi kuwa na tatizo hilo la moyo wala maumivu ya aina yoyote hadi lilipotokea ghafla.

Marco ameacha mke na watoto 4. Ibada ya kuaga mwili itafanyika leo Agosti 22, 2024 saa 11 jioni Hospitali ya Taifa Muhimbili mwili utasafirishwa kuelekea Kahama kwa ajili ya mazishi ambayo bado tarehe haijatajwa.

Marco akiwa na kundi la Zabron Singers walitamba na vibao kama Mkono wa Bwana, Sweety Sweety, Upo Single, Nakutuma wimbo na nyingine nyingi