Mama wa Ney wa Mitego wakataliwa na Basata

Tuesday May 04 2021
ney pic
By Nasra Abdallah

Wakati jana msanii Ney wa Mitego ilikuwa aachie wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘mama’ kama alivyowahidi mashabiki zake, imeshindikana baada ya Baraza la Sanaa a Taifa kukataa usiende hewani mpaka pale utakapofanyiwa marekebisho.

Hayo yamebainika jana Jumatatu Mei 3,2 021, baada ya msanii huyo kuweka wazi jambo hilo kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram

Ney ambaye jina lake halisi ni  Emmanuel Elibariki, aliandika ”Leo ilibidi nitoe wimbo wa ‘mama’ kama ambavyo niliwaahidi lakini imekua ngumu kuutoa nimeupeleka Basata, wameukataa.

“Wameniambia una ukakasi unahitaji marekebisho na mimi kwa upande wangu siwezi kubadilisha sababu mpaka sasa gharama nilizotumia ni kubwa sana na video ipo tayari kwa hiyo sitoweza tena kuutoa huo wimbo,”ameandika Ney.

Mwanaspoti imewatafuta Basata kujua ukweli wa jambo hili, ambapo kupitia Kaimu Katibu Mtendaji wake, Matiko Mniko alikiri kuwa wameupokea na kuupitia wimbo huo na kubainisha kuwa walimuagiza akarekebishe baadhi  ya mistari lakini sio kwamba wameukataa.

Advertisement