Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makosa yanayofanywa na wasanii wengi Bongo

Muktasari:

  • Yapo makosa ambayo baadhi yao wanayafanya na kinachotokea ndiyo majibu ya hayo maswali na mengi mengine yanayofanya hadi wengine kufilisika kimuziki kutokana na kukosa mwendelezo.

UNAJIULIZA kwa nini wasanii wengi wanapotea kwenye ramani ya muziki? Kwa nini wasanii wengi hawatoboi nje ya mipaka ya nchi, yaani kimataifa na kubaki na masoko ya ndani? Unajiuliza kwa nini baadhi ya wasanii wameanza kuchokwa na mashabiki wao na kujikuta hata shoo zao tu hawafiki na hawasikilizi ngoma zao?

Yapo makosa ambayo baadhi yao wanayafanya na kinachotokea ndiyo majibu ya hayo maswali na mengi mengine yanayofanya hadi wengine kufilisika kimuziki kutokana na kukosa mwendelezo.

Nini kinawafelisha? Hapa Mwanaspoti linakuchambulia mambo 10 ambayo kwa namna moja au nyingine ndiyo yanaleta shida kwa wasanii na kupoteza mvuto katika jamii ikiwamo mashabiki wao.


1. Ngoma baada ya ngoma

Hii inachangia kwa kiasi kikubwa kwani wasanii licha ya kufurahia kutoa nyimbo nyingi lakini inachosha mashabiki. Msanii anatakiwa kuangalia soko. Msanii anatakiwa atoe nyimbo kwa kuangalia na wakati sahihi ili kuwateka mashabiki kuliko kuwajazia nyimbo hadi zinawachosha.

Msanii anatakiwa awe na ratiba ya kazi zake. Asome mashabiki wake wanataka nini na kwa wakati gani na siyo kutoa tu ngoma kisa una uwezo wa kuingia studio. Inaboa.


2. Matumizi ya teknolojia

Hakuna ubishi kwa sasa dunia imehamia katika teknolojia na kinachofanyika ni wengi kugeukia huko. Hakuna namna lazima wasanii waendane na teknolojia ikiwamo matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii ili kujitangaza zaidi hasa kazi zao.

Ili kazi ya msanii ifike mbali lazima ashirikishe hii mitandao ikiwamo Instagram, X, Facebook ambayo ina watumiaji mamilioni na waonapo kazi nzuri inasaidia msanii kuendelea kufuatiliwa. Hapa wasanii wengi bado hawajaamka.

3. Ushirikiano na vyombo vya habari

Kama ilivyo namba mbili, hapa ni muhimu zaidi. Msanii anaweza akaandika kuhusu maisha yake katika mitandao ya kijamii, ni sawa, ila huku kwenye vyombo vya habari kuna umuhimu wake kwa msanii kupazingatia.

Kuna wasanii hawapendi kufanyiwa mahojiano na vyombo vya habari ilhali ndiyo pekee vinavyofuatiliwa na wengi zaidi ya mitandao ya kijamii. Huku kunamsaidia msanii nyimbo zake kupigwa au kuandikwa na kuzidi kutangazwa. Amkeni.


4: Wengi hawana usimamizi mzuri

Hii ni shida. Na ndiyo maana wasanii wengi wakitoka ndani ya muda mfupi wanapotea. Unakuta meneja anamsimamia msanii kwa masilahi yake. Akifanikiwa na akiona msanii anayumba, anaomndoka anamtafuta mwingine. Wasanii wanatakiwa wajanjaruke kwenye hili, kwenda sambamba na mameneja na wasimamizi wengine ikiwamo mambo ya kimkataba ili kumfanya meneja asimdhulumu.

Mameneja wengi unakuta hawana ufahamu na muziki na kinachowabeba ni pesa zao, hii inachangia kwa kiasi kikubwa wasanii wengi hasa wachanga kufeli mapema. Ni lazima msanii asimamiwe na meneja anayeelewa muziki ikiwamo njia za mafanikio ya msanii, fitina za wasanii wengine na namna ya kumsimamia msanii wake.


5. Kiki/kashfa sio poa

Wasanii wengi hawajui, kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza. Kama kazi ni nzuri kwa nini isiuze. Kama una uhakika na unachofanya kwa nini ufeli. Hapa ndipo wengi wanaona njia pekee ya kufikia mafanikio yao ni kufanya mambo ya ovyo kwanza, waswahili wanasema 'Kiki'. Zinasaidia nini?

Kwa mwanzo zilikuwa na faida na ziliwafanya mashabiki kutaka kujua kinachoendelea na mwishoni ni kazi imeachiwa. Kwa sasa kiki hazina kiki tena, hivyo wasanii watumie tu kazi zao. Kama ni nzuri itajipaisha yenyewe na kama haijakubalika ni kukaza tu. Msipende mambo ya mkato.

6. Kuigana

Hapa ndipo panakera zaidi. Wasanii wengi sio wabunifu na mara nyingi kazi zao zinafanana. Achana na kuiga kutoka mataifa mengine kama ilivyo kwa Amapiano kutoka Sauzi. Hapa tu nchini wengi wanapita na upepo wa wenzao. Sababu ninini? Hakuna ubunifu.

Nyimbo zikipigwa unashindwa kuutambua huu ni wa msanii gani kwa sababu zinafanana kuanzia midundo, mashairi na hata wakati mwingien video. Kwa nini hakuna ubunifu? Badilikeni.


7. Ushawishi, ukaribu kwa jamii

Kuna baadhi ya wasanii wakitoa nyimbo fasta tu zinawafikia mashabiki wao na wanatoa sapoti kubwa sana kwao. Siyo tu bahati, ni kwa sababu wana uwezo wa kuwafanya wawakubali. Kivipi? Msanii anakuwa karibu na mashabiki zake kwa namna moja au nyingine. Anakuwa karibu na jamii inayomzunguka na hata nje ya eneo lake. Kujitoa kwa ajili ya mashabiki na jamii inakupa nafasi kubwa ya kukubalika na hata ukitoa nyimbi ni lazima wazifuatilie.

Mfano mzuri ni Mfalme wa Pop, Michael Jackson, ndiye msanii aliyewahi kupendwa na watu wengi zaidi duniani enzi zake, siyo kwa sababu ya kazi zake, bali kwa sababu ya ushawishi wake ikiwamo kuwa karibu na jamii.

Nani ataenda katika shoo ya msanii ambaye hashawishi? Ni ngumu. Wasanii wanatakiwa kuwa wabunifu na wenye ushawishi katika jamii.


8. Video 'vichupa' duni

Kuna mambo mengine haina haja ya kulazimisha. Wanasema starehe gharama, maana yake ni kila kizuri lazima kigharamiwe. Kwenye kutoa video za nyimbo wasanii wengi wanatuangusha. Unakuta mashairi ya nyimbo hayaendani na video. Ni kweli wimbo unaohusu huzuni msanii aonekane klabu?

Msanii anaimba maisha ya shida kwenye BMW? Hii siyo sawa. Wasanii wanatakiwa wajue nyimbo zao ndiyo mwongozo wa video (Script).

Msanii ili kuwa na video bora pia lazima afanye uwekezaji mkubwa.

9. Mashairi yasiyo na mpango

Inafurahisha sana. Msanii anaandika nyimbo na mashahiri hayana mpangilio. Stori haina mwendelezo na haina maudhui yanayoeleweka. Matumizi pia ya lugha yanachangia kuufanya wimbo kupoteza ladha kwa mashabiki na kusababisha pia kuishia kufungiwa na mamlaka zinazohusika na usimamizi wa kazi zao.

Ni wazi mashabiki wamechoka matusi, kufungiwa kazi isiwe kiki, kuitwa sana Basata isiwe sehemu ya kutafuta umaarufu. Kwa upande mwingine mashabiki wanadharau kazi zako na mwishowe unalaumu haupati mafanikio kumbe njia unazopita sizo. Wasanii wabadilike.