Lulu na Majizzo wapata mtoto wa kiume

Saturday July 17 2021
lulu pic
By Nasra Abdallah

Msanii anayetamba katika tasnia ya filamu, Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu ajifungua mtoto wa kiume.
Taarifa hizo zimethibitishwa leo Jumamosi Julai 17, 2021 na mme wake  Francis Ciza ’Majizo’ kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram.
Katika ujumbe wake huo, Majizo ameandika, ”Ililibaki kama jina la kufikirika, mimi na Mama yake tulikuwa tunalitumia (Baba G/Mama G) wakati mtu mwenyewe hayupo.

“Lakini imani ni kuwa na hakika na mambo yanayotarajiwa, tulikuwa na imani kwa Mungu wetu kwamba ipo siku bwana ‘G’ atakuja duniani. Mungu amejibu maombi yetu, mimi na mke wangu Elizabeth tumejaaliwa mtoto wa kiume, jina lake ni ‘G’.

“G na mama yake wako vyema kabisa kiafya, tumejawa na furaha kubwa. Namshukuru mke wangu kwa zawadi hiyo.Baasi tukumbukane katika sala na dua zenu. Asanteni.
Lulu na Majizo walifunga ndoa Februari 16 mwaka huu, ndoa iliyokuwa ya siri na ilihudhiriwa na watu wachache wa karibu yao.

Advertisement