Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Luiza Mbutu afiwa na baba mzazi

LUIZA Pict

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti, Luiza amesema, baba yake amefariki kwa saratani ya koo wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Kitengule iliyopo Tageta jijini Dar es Salaam.

Siku chache baada ya kufiwa na mumewe Fariala, mkurugenzi mtendaji wa bendi ya muziki wa dansi ya Twanga Pepeta, Luiza Mbutu, amefiwa na baba yake mzazi leo, Jumatatu Januari 12, 2026.

Akizungumza na Mwanaspoti, Luiza amesema, baba yake amefariki kwa saratani ya koo wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Kitengule iliyopo Tageta jijini Dar es Salaam.

"Baba yangu amefariki dunia leo jioni. Alikuwa akipatiwa matibabu ya saratani ya koo. Mpaka umauti unamkuta alikuwa akipatiwa matibabu Hospitali ya Kitengule, hivyo tunaendelea kufanya taratibu za mazishi nyumbani kwangu Salasala," amesema Luiza.

Desemba 25, 2025, Luiza alifiwa na mumewe Fariala Mbutu akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuugua kwa wiki moja.

Luiza amesema, Fariala alikuwa anasumbuliwa presha, lakini ghafla alipata tatizo la tumbo ambalo ndilo lililochukua uhai wa mumewe.

"Alikuwa anasumbuliwa na presha tu, ila akaja kuumwa tumbo ghafla likavimba, tukampeleka Hospitali ya Muhimbili akafanyiwa vipimo akakutwa na tatizo la mrija wa kupitisha chakula umevimba, ikabidi wamfanyie upasuaji wakapunguza utumbo kisha wakaunganisha tena akawa anaendelea na matibabu ndio akafariki...," amesema Luiza.