Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Linex awashtukia kauzibe

Muktasari:

  • Staa huyo wa ngoma kama 'Salima', 'Wema kwa Ubaya',  'Moyo wa Subira' na nyingine aliliambia Mwanaspoti tofauti na yeye ambaye anawapenda na kuwasapoti wenzake, wasanii wengi hawashirikiani kwa lolote na hiyo ni ishara ya chuki na kukosa upendo, kitu kinachorudisha nyuma muziki wa Bongo.

MSANII wa Bongo Fleva, Sunday Mjeda 'Linex' amesema sio wasanii wote wana moyo wa kusapoti na kuwapenda wenzao, huku akidai kwenye fani wapo kauzibe kibao wasiopendana bila sababu.

Staa huyo wa ngoma kama 'Salima', 'Wema kwa Ubaya',  'Moyo wa Subira' na nyingine aliliambia Mwanaspoti tofauti na yeye ambaye anawapenda na kuwasapoti wenzake, wasanii wengi hawashirikiani kwa lolote na hiyo ni ishara ya chuki na kukosa upendo, kitu kinachorudisha nyuma muziki wa Bongo.

"Inashangaza sana, kuna baadhi ya wasanii wenzangu wanaishi kama hawahitaji tena wengine maishani mwao, wakati ukweli katika maisha kila mtu anamhitaji mwenzake, kwani hata maji machafu husaidia kuzima moto," alisema Linex na kuongeza ifike wakati wasanii kupendana na kupigana tafu kwa hali na mali.

"Tusiwe tunasubiri katika misiba tu ndiyo tujifanye tunaonyeshana upendo, tupendane na kusaidiana tukiwa hai kwani kila mmoja atafurahia upendo na msaada huo, mtu akiwa katika jeneza haisaidii kama ulishindwa kumjali akiwa hai. Tubadilike kwa manufaa ya hili gemu," aliongeza Linex.