Leo ni miaka 37 tangu Bob Marley afariki

Muktasari:
Katika enzi za uhai wake, Bob Marley alipata umaarufu na mafanikio zaidi kupitia nyimbo zake tofauti zenye miondoko hiyo ya lege zilizotokisa anga la muziki ulimwenguni haswa kutokana na nyimbo zake nyingi kutetea haki za binadamu na kupinga ukoloni.
Msanii wa lege (reggae), Robert Nesta Marley maarufu zaidi kwa jina la Bob Marley, amefariki tarehe kama ya leo ya Mei,11, 1981 katika hospitali ya University of Miami iliyo, Miami, Florida, Marekani.
Katika enzi za uhai wake, Bob Marley alipata umaarufu na mafanikio zaidi kupitia nyimbo zake tofauti zenye miondoko hiyo ya lege zilizotokisa anga la muziki ulimwenguni haswa kutokana na nyimbo zake nyingi kutetea haki za binadamu na kupinga ukoloni.
Baadhi ya nyimbo zake ni, Africa Unit, Redemption Song, Buffalo Soldier, Three Little Birds, Exodus, Soul Rebel, Get Up, Stand Up, Satisfy My Soul, Stir It Up na Is This Love
Bob Marley ambaye ameacha watoto 11, amefariki akiwa na miaka 36 kwa ugonjwa wa Melanoma (saratani ya ngozi) na leo ni miaka 37 tangu kifo chake.