Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa mitoko ya usiku, ndio yenyewe hasa

YAANI hii si ya kuikosa katika kabati yako ati. Maana haiishi fasheni na inapendwa sana kuvaliwa na kinadada hasa katika mitoko, usiku na sherehe mbalimbali kama harusi.

Aina hii ya nguo hurusuhu sehemu kubwa ya mabega yako na mgongo kuonekana. Ni aina ya nguo ambayo hupendwa kuvaliwa sana kipindi cha joto.

Maharusi wengi pia hupenda kuvaa magauni yaloshonwa mabega wazi na kiukweli huvutia sana. Sasa hebu leo tuangalie ni jinsi gani unaweza kuvaa gauni au blauzi iloshonwa mabega wazi na je ni wakati gani sahihi na sehemu sahihi unapaswa kuvaa nguo aina hii.

Aina hii ya mavazi huvutia zaidi ikivaliwa katika mitoko au sherehe mbalimbali hasa kama nilivyotangulia kusema hapo juu, vaa aina hii ya nguo katika harusi, kicheni pati au hata katika sendoff.

Nguo hizi hupendeza zaidi kwani ni rahisi kuzinakshi na mablingbling kama cheni kubwa na hereni ili kuvutia zaidi.

Pia aina hii hufaa ikivaliwa kama una toka ‘out’ labda katika fukwe za bahari ila hapa hupendeza kama ukitupiamo blauzi aina hii na kaptula au suluwali aina ya jinsi au sketi fupi ama sketi nyepesi na ndefu.

Waweza vaa aina hii ofisini ila angalia lazima utupiemo kijikoti ili usionyeshe mwili wako sehemu za kazi. Au ukivaa aina hii kumbuka kutoruhusu nguo yako ya ndani kuonekana.

Aina hii ya nguo si nzuri kuvaa katika nyumba za ibada ndio maana hata maharusi wakivaa katika nyumba za ibada uhakikisha wamejitupia mtandio ili kutoruhusu sehemu ya mwili wao kuwa wazi.

UTUPIE NINI

Kama umevaa aina hii ya blauzi katika mitoko yako ya beach na matembezi ya kawaida waweza kutupia kiatu simpo au Sandozi yoyote ile itakayokufanya uwe huru kuzurura.

Kama ni mitoko ya usiku kama sherehe, basi jitupie mchuchumio wa maana. Ikitokea umevaa ofisini basi wedges ndio mahala pake.