Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kuna nini? Johari, Chuchu Hans washtua

Muktasari:

  • Mwanaspoti ambalo lilialikwa kwenye sherehe moja na kuwakuta wasanii hao lilishuhudia tukio hilo ambalo lilishtua hata waliokuwepo karibu ya wawili hao kutokana na kilichokuwa kikiendelea.

LINAACHA maswali... Ndiyo, ni tukio la wasanii wawili wakali wa Bongo Movie, Johari Chagula na Chuchu Hans lililotokea wiki iliyopita Mikocheni, jijini Dar es Salaam.

Mwanaspoti ambalo lilialikwa kwenye sherehe moja na kuwakuta wasanii hao lilishuhudia tukio hilo ambalo lilishtua hata waliokuwepo karibu ya wawili hao kutokana na kilichokuwa kikiendelea.

Ni hivi. Katika sherehe hiyo fupi, Chuchu Hans akiwa ni mmoja wa waliokuwa wakihudumia wageni waalikwa, hivyo hakuisha kupitapita na mmoja wa wageni aliyekuwa karibu na Johari, alitaka maji na ndipo alipotaka Chuchu ashhtuliwe ili ampatie kinywaji hicho.

Sasa bana, mgeni huyo si ndo akamgusa Johari amshtue Chuchu. Ndipo hapo mshangao ukampata mgeni huyo na mwandishi wa Mwanaspoti na kama ilivyo kwa wengi wanajua wawili hao hawakuwa na tatizo baina yao ‘bifu’.

Kilichotokea ni Johari alipoona ameombwa amshtue Chuchu alibadilika na kuonyesha kukerwa na jambo hilo.

Hivyo, Johari aligoma  huku akimpa onyo mgeni huyo asirudie tena kumuhusisha na na Chuchu.


Mwanasapoti Kazini

Mwanaspoti baada ya kuona tukio hilo, ilibidi awatafute wawili hao ili kujua ukweli kama bado hawana uhusiano mzuri au kuna jambo lingine.


Johari

“Mimi sitaki sitaki sitaki...(Anataja jina la mwandishi), haya mambo kuzungumza hapana kwa kweli embu niache, kwa nini nizungumze na mtu kwani kuna ulazima gani? kila mtu ana maisha yake bana sitaki nihusishwe na huyo mtu, mimi nipo ‘busy’ na kazi zangu sasa hivi umeona napungukiwa na kitu?”


Chuchu Hans

“Mimi hapana, niko bize na mambo yangu sifuatilii ya mtu mwingine, nani ameniongelesha nani hajaniongelesha, na sio lazima kuongea na kila mtu, ila mimi nachojua sina tatizo na mtu, labda kama mtu ana matatizo na mimi na kwa nini nianze kumzungumzia mtu sasa hivi kwa mambo yaliyopita kitambo?”


Tujikumbushe

Kipindi cha nyuma, Johari alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Ray, uliosababisha wawili hao kuanzisha kampuni yao inayojishughulisha na mambo ya filamu ya RJ Company.

Hata hivyo, ghafla Chuchu Hans alianza kuonekana akiwa na ukaribu na mwanamume huyo, kitendo kilichosababisha kuwepo na kutokuelewana kati yao kulikodumu kwa muda mrefu.

Inadaiwa pia, Chuchu alibadilisha jina la kampuni ya RJ nakuiita Rjaden (akimaanisha Ray na mwanaye aliyezaa na Chuchu aitwaye Jaden).

Kitendo hicho kilizidi kumchukiza Johari na kuzidi kutoelewana.

Hata hivyo, baadaye ilionekana hali ya mambo imetulia lakini kwa kilichotokea wiki iliyopita baina yao, ni wazi wengi wanajiuliza kwani kuna nini na kama ni bifu litaisha lini na nani atalimaliza? Tusubiri tuone.