Kumbe Paula umaarufu ulimfuata
Muktasari:
- Paula alisema baada ya kuingia kwenye mtandao wa Instagram kwa kupostiwa na mama yake, watu wakaanza kumshambulia umri wake mdogo na wengine kusema ni mwanafunzi ndiyo umaarufu wake ukakua zaidi.
MTOTO wa mwigizaji Kajala Masanja, Paula amesema katika maisha yake yeye ndiye aliyeutaka umaarufu na umaarufu ukamfuata wenyewe kutokana na kupostiwa na mama yake kwenye mtandao wa Instagram.
Paula alisema baada ya kuingia kwenye mtandao wa Instagram kwa kupostiwa na mama yake, watu wakaanza kumshambulia umri wake mdogo na wengine kusema ni mwanafunzi ndiyo umaarufu wake ukakua zaidi.
"Mimi niliutaka umaarufu na wala watu wasimlaumu mama yangu kwa kumwambia amenilea vibaya, nilikuwa napenda mama akiniposti nafurahi, ila baadhi ya watu walikuwa wanamshambulia mama kwa kuona amenilea katika maadili mabaya, nikawa najiuliza kwani mtu ukipostiwa kwenye mitandao ndio unakuwa na tabia mbaya? Sasa yale mashambulizi yao ndiyo nasema umaarufu ulinifuata baada ya kuwa instagram nikajulikana, lakini baada ya kuwa maarufu nikabadilisha maisha yangu na kutulia katika mahusiamo yangu na kupata mtoto," amesema Paula.
"Kama una nyota ya kujulikana na kuwa staa utajulikana tu, huwezi kuzuiliwa kwa chochote, sababu ya kuwa staa nayo ni kazi, siyo kila mtu anaweza, kuwa nacho hiko ni kapaji, ndiyo maana kuna wengine wanafanya mambo yasiyo na maadili yakutaka wawe maarufu," ameongeza.