Kesi ya mume wa Osinachi yaunguruma mwezi mmoja, ahukumiwa kunyongwa

Wednesday June 08 2022
mwimbaji pic

Osinachi Nwachukwu

By Nasra Abdallah

Aprili 9, mwaka huu haikuwa siku nzuri kwa mashabiki wa msanii wa nyimbo za injili nchini Nigeria, Osinach Nwachukwu, baada ya kusambaa kwa taarifa za kifo chake.

Msanii huyo licha ya kutamba na nyimbo mbalimbali lakini wimbo uliompa umaarufu zaidi ni ule wa ‘Ekwueme’ alioimba kwa kushirikishwa na mchungaji Prospa Ochimana ambao mpaka sasa umeshatazamwa mara milioni 78 kwenye mtandao wa YouTube.

Hatimaye haki imetendeka baada mume wake kukutwa na hatia ya kuhusika na kifo cha msanii huyo na mahakama kuamuru anyongwe hadi kufa.

Kesi hiyo imechukua takribani mwezi mmoja kunguruma kwake hadi kutolewa hukumu.


Hali ilivyokuwa

Advertisement

Awali sababu za kifo cha Osinach zilielezwa kuwa ni kansa ya koo, lakini familia ilipinga taarifa hizo ambapo baadaye hospitali ya Taifa ambapo umauti ulimkuta ilifanya uchunguzi wa mwili wake na kukabidhi ripoti kwa polisi.

Licha ya Polisi kutoweka hadharani majibu hayo, lakini za kutoka ndani ya familia zilisema marehemu alikutwa na uvimbe wa damu ulioganda kwenye kifua uliopelekea kifo chake,hali iliyotakana na kipigo kutoka kwa mumewe Peter Nchachukwu .

Juni 4, Peter alipandishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka 23 kati ya hayo yanahusiana na unyanyasaji wa nyumbani,unyanyasaji wa kihisia na kisaikolojia na kuua bila kukusudia.

Siku moja iliyopita mahakama ilimkuta na hatia mwanaume huyo na kumuhukumu kunyongwa hadi kufa ambapo ukipiga hesabu ya namna ya kesi hiyo ilivyoendehwa kwa haraka imechukua mwezi mmoja tangu ilipoanza kunguruma na miezi miwili kasoro siku mbili tangu kutokea kwa kifo cha Osinachi Mwisho.

Advertisement