Jux, Priscilla wapata mtoto wa kiume, ataitwa Prince Rakeem
Muktasari:
- Taarifa hiyo imetolewa kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ya mwanamuziki huyo na mke wake Priscilla wakichapisha picha, majina ya mtoto wao na tarehe aliyozaliwa ambayo ni Agosti 24, 2025.
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Juma Mkambala 'Jux' na mke wake Priscilla wamebarikiwa kupata mtoto wao wa kwanza wakiume aliyezaliwa huko nchini Canada na kumpatia jina la Rakeem Ayomide Mkambala.
Taarifa hiyo imetolewa kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ya mwanamuziki huyo na mke wake Priscilla wakichapisha picha, majina ya mtoto wao na tarehe aliyozaliwa ambayo ni Agosti 24, 2025.
Mama na mtoto wanaripotiwa kuwa na afya njema, na familia inasemekana kuwa na furaha huku wakisherehekea hatua hii muhimu katika maisha yao.
Rakeem ambaye anakuwa mtoto wa kwanza kwa wawili hao ambao walifunga ndoa Februari 7, 2025, nyumbani kwa mwanamuziki huyo Mbezi, Jijini Dar es Salaam.
Mwaka mmoja umetosha kuleta matunda katika mahusiano ya wa wili hao, ambayo yalianza mapema mwezi Agosti, 2024, baada ya kukutana nchini Rwanda, huku penzi lao likishamiri na kuteka mitandao ya kijamii ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.