Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mzee Yusuf: Wasanii acheni unafiki

MZEE Pict

Muktasari:

  • Mzee Yusuf ambaye ni mmiliki wa bendi ya Jahazi Modern Taarab na mwimbaji, aliwahi kutamba na nyimbo kama ‘Mpenzi Chocolate’, ‘Wasi wasi wako’, ‘Nakula kwa Nakshi’, ‘Tupendane’ na nyingine nyingi.

GWIJI wa muziki wa taarabu nchini, Mzee Yusuf amesema wasanii wengi ni wanafiki ndiyo maana wengi wao hawana mafanikio.

Kwenye mahojiano na Mwanaspoti Mzee Yusuf alisema, “Leo niwaombe sana wasanii Watanzania, unafiki ndiyo unatufikisha hapa tulipo, ukiona msanii mwenzako anaandaa kitu msapoti kwa njia zozote unazoweza ili kesho na wewe ukiwa na cha kwako na yeye akusapoti ingawa wasanii wa Bongo unaweza ukamsapoti ikifika zamu yako anakausha, anasubiri mpaka anapokuja tena anaomba umsapoti, sasa huo ni unafiki.”

Mzee Yusuf ambaye ni mmiliki wa bendi ya Jahazi Modern Taarab na mwimbaji, aliwahi kutamba na nyimbo kama ‘Mpenzi Chocolate’, ‘Wasi wasi wako’, ‘Nakula kwa Nakshi’, ‘Tupendane’ na nyingine nyingi.

Pia ni mtunzi, mpiga kinanda na Gitaa, nyimbo ambazo amewahi kutunga ni pamoja na ya Khadija Yusuf ‘Nilijua Mtasema’ wa Mwanahawa Ally ‘Roho mbaya’ ‘Hayanifiki’ wa Isha Mashauzi, ‘Mkuki kwa Nguruwe’ wa Leila Rashid na nyingine nyingi.