Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Anko lao ... Majibu Konki

Muktasari:

  • Jibu: Hili ndilo tatizo la kula kulala...yani pamoja na anko'ako kuhifadhi katika umri huo uliopaswa ujitegemee na kuwa na kwako, bado umefikia hatua ya kumzengea bintie wa kazi...jisikie aibu kidogo au utazifanya kazi anazozifanya utakapomhribia hapo home? Ebu acha zako buana...pambana utoke kwanza hapo home ndio uanze ubazazi wako!

1. ANKO Lao, kijana miaka 22, nimetokea kumpenda mfanyakazi wa uncle wangu ni mrembo kweli. Nifanyeje nimnase?

Hamidu, Dodoma


Jibu: Hili ndilo tatizo la kula kulala...yani pamoja na anko'ako kuhifadhi katika umri huo uliopaswa ujitegemee na kuwa na kwako, bado umefikia hatua ya kumzengea bintie wa kazi...jisikie aibu kidogo au utazifanya kazi anazozifanya utakapomhribia hapo home? Ebu acha zako buana...pambana utoke kwanza hapo home ndio uanze ubazazi wako!


2. ANKO Lao, mwanamke miaka 35 nina mtoto mmoja wa miaka 10, lakini sijazaa na mume wangu ninaeishi naye kwani niliyezaa hakuwa riziki, ila tabia ya mwenzangu ni kutoa hela ya kula isiyozidi wala kupungua licha ya kumueleza maisha yamebadilika hanielewi. Nifanyeje?

Mamy, Chanika


Jibu: Sijajua unaachiwa kiasi gani cha fedha kiasi cha kutokutosheleza, ila kama kweli ni mumeo ni unakijua kipato chake kama unadhani anakuzingua, zungumza naye. Lakini, baba mzazi wa huyo dogo uliyenaye yu wapi, kwani huenda mumeo hana furaha ya kuhudumia damu ya wenzake, wakati yeye hana chake hapo! Wanaume wana hisia nao kama nyie mkiletewa mtoto asiyewahusu!


3. ANKO Lao, kijana miaka 22 nimeachana na aliyekuwa mpenzi wangu miezi sita iliyopita tangu tuanze uhusiano, imepita miezi kadhaa sasa, lakini nimeshindwa kumsahau. Nifanyeje?

Haruna Ally, Dar


Jibu: Huo muda unaotumia kumuwaza mtu asiye na mpango nawe, si ungetumia kuitengeneza kesho yako kwa kusaka maokoto. Inaonekana ni wazi umetemana na bibie huku ukiwa bado unampenda. Jaribu  kumpotezea kwa kusaka noti wewe, utakufa kwa stresi wakati mwenzako ananenepa huko!


4. ANKO Lao, kijana miaka 24 nina mke nimeza naye mtoto mmoja, ila tunashindwa kuelewana kwani amekuwa mbishi na kunitukana akiwa pia na wivu mkali hadi kero. Nifanyeje?

Jackson Japhet, Mvumi Dodoma


Jibu: Ama vijana wa zama hizi miyeyusho sana, yaani unapelekeshwa na kitoto cha mwaka 2000! Ni wazi kuna mambo unayafanya na kumtibua mwenzako, kwani ni ngumu mke anayemheshimu mumewe na kutoa shombo hata kama ana wivu mkali. Wee jitathmini, la sivyo ndoa itakushinda!


5. ANKO Lao, kijana miaka 33 nilikuwa na mpenzi niliyejitoa kwake nikiwa na lengo la kumuoa na nilitaka kwenda kujitambulisha kwao, lakini alinizuia akisema kuna mambo anayaweka sawa kwanza, cha ajabu alinibadilikia na mawasiliano yakawa hafifu, mwishowe nakuja kuona status picha za harusi yake. Ni kweli alikuwa ananipenda huyu?

Shafii Omary, Temeke Dar


Jibu: Ni kweli kusoma hujui, lakini picha nayo ilikutatiza kiasi cha kushindwa kuielewa? Kwamba huyo bibie wala hakuna na ishu nawe, ila we ulijibebisha kizoba...kilichokupata ni somo ili siku nyingine usiingie kiboya katika malavidavi hasa mademu wa Dar...Pole yako!


6. ANKO Lao, kijana miaka 28 nimekuwa nikipambana na maisha, lakini nimekuwa nakwama kutokana na kusumbuliwa na ulevi wa pombe, Napambana kuacha, ila nashindwa, huku umri unaenda na ninahitaji kuwa na familia ila ulevi unanikwamisha. Nifanyeje?

Patrick, Dodoma


Jibu: Kama ulivyojifunza kunywa pombe, ndivyo unavyotaka kupambana kuiacha kwani, huo sio ulemavu ila kujiendekeza na kupenda kuishi maisha ya kuiga. Zipo dawa za kisuna zinazosaidia mtu kuacha ulevi, lakini kikubwa ni wewe mwenyewe kukata shauri na kuacha kwani pombe hazijawahi kuwa na manufaa kwa mtumiaji zaidi ya kupoteza fedha na kuharibu afya na malengo. Kazi kwako!


7. ANKO Lao, kijana miaka 27 kuna lishangazi limetokea kunipenda, ila simpendi hata kidogo na nishalieleza kuwa mimi tayari nina mtu wangu, lakini hanielewi. Nifanyeje?

Elias Makamba, Chanika


Jibu: Mwenzio kafa na kuoza juu yako ndo maana haelewi somo...ila sioni kwa nini unakuwa kaksi namna hiyo na kumbania mwenzio...au unamuona ni mbibi saba? Kama upo siriazi mpashe ukweli ukionyesha sura ngumu, la sivyo ataendelea kukuganda...hujui ana-misi nini huyo. Kazi kwako!


8. ANKO Lao, binti miaka 25 nina mpenzi ninampenda, lakini hajatulia kwani nimebaini ana mtu mwingine japo nikimuuliza anamkana. Nifanyeje?

Zaitun Adam, Mafinga


Jibu: Kama umeshagundua jamaa hajatulia we unakomaa naye kwa kazi gani au unapenda kufa mapema kwa stresi na maradhi?! Ni vyema ukamuepuka mapema kwa kumpiga chini, kwani hujui ana wangapi usiowajua na kwa dunia ya sasa utajiweka pabaya wakati wajomba watulivu wapo!


9. ANKO Lao, kijana miaka 27, tatizo langu kila nikilipwa mshahara, pesa haikai kwa sababu ya madeni mengi niliyonayo. Nifanyeje nitoboe?

Rafael Isaac, Mwanza


Jibu: Huwezi kutoboa kama unachotumia ni zaidi na unachokiingiza...punguza matumizi pia acha kujimwambafai wakati pesa yako ni ya mawazo. Pia usisikilizie sanaa mshahara, kwani haujawahi kutosha. Ni vyema ukatengeneza mipango ya kuwa na mishe nje ya kazi  ikuingizie fedha! Hivyo tu!


10. ANKO Lao, binti miaka 28, ni muda mrefu nimekuwa nikisaka mchumba ili aje kuwa mume, ila mambo yamekuwa magumu. Sielewi tatizo nini, naomba ushauri, nifanyeje?

Stellah H.K, Morogoro


Jibu: Lazima ujue kwanza kwanini masela wanapita nawe kisha wanakukaushia! Kama hujatulia, mjuaji mwingi na usiye na haiba za kike, basi ujue mapema utazeekea kwenu! Ushuri wangu jitathmini kwanza mwenyewe ujue wapi unakosea, pia ikiwezekana hama hapo ulipo, kwani huenda umezoeleka sana! Wakati mwingine unajinyima riziki kwa kukaa sehemu moja kama utumbo!


11. ANKO Lao, binti miaka 20 kuna mtu ananipenda sana, ila simpendi kwa sababu sioni kama ananifaa kwa maisha ya kufa na kuzikana. Nifanyeje?

Moureen Ismail, Dodoma


Jibu: Thamani ya kitu huwezi kuijua hadi itakapokuponyoka, kwani unachokifanya kwa sasa wewe ni kama kupiga teke fuko la pesa na  si unajua mchagua nazi hupata koroma...mpotezee huyo jamaa, lakini utamkumbuka pale utakapozeekea homu bila ya nd0a kwa mashauzi uliyonayo. Shauri yako!


12. ANKO Lao, kijana miaka 23 kuna binti tunapendana ila amekuwa mgumu kuachia mzigo, akisema eti hadi tutakapokuja kuoana, wakati najua alishapita na mtu kabla yangu. Nifanyaje?

Eric Kandoro, Ilula Iringa


Jibu: Huyo bibie ni mtu anayejielewa, ameshtuka kosa alilofanya awali, akijua akibugi tena itakula kwake. Kama kweli una nia ya dhati fanya chapu upeleke posa na kuoa kabisa ili ujipakulie pilau nyama nyingi na sio kuleta usela kwa kutaka kutembea na nyota ya mwenzio. La sivyo jiongeze!


12. ANKO Lao, kuna binti nampenda ila shida yake kubwa ni kwamba haniamini hata kidogo akidhani nataka kumchezea, wakati nipo siriazi naye. Nifanyeje?

Amir Salum, Tanga


Jibu: Inategemea na nyendo zako na gia ulizomuingia wakati unamtokea. Cha kufanya zungumza naye na kumueleza ukweli atulize moyo, lakini kwa kuharakisha kutuma washenga kwao ili ufanye chapu umuoe na kama una macho mia mia, basi jitathmini la sivyo utaachwa solemba! Kazi kwako


13. ANKO Lao, binti miaka 21 naishi na mwanamume aliyenizidi umri ila mambo yake anayofanya ni kama vile ana mchepuko, kiasi ananinyima raha kabisa. Nifanyeje?

Rachel Edson, Singida


Jibu: We mwana unaa kiranga, katika umri huo tayari umeanza kuneng'eneka hadi kujipeleka geto la mbabu? Kama umeshagundua ana mademu wengine we unasubiri nini kumtema au unataka upewe kidudu uhangaike nacho? Kwa umri ulionao ungetafuta saizi yako uolewe maisha yaendelee.


14. ANKO Lao, kijana miaka 26 naishi na mpenzi ninayempenda sana, ila tatizo ni kwamba huwa  tunagombana kila mara kwani hataki kuona nikichati kupitia simu, nami nina marafiki. Nifanyeje?

Athuman Miraj, Chalinze


Jibu: Hili ndilo tatizo la kuvamia malavidavi kabla ya maandalizi, we ushajua mwenzako hapendi jambo hilo, kitu gani kinachokufanya uendelee kumkera au braza bibie kalazimisha kuzama getoni, hivyo unatengeneza mazingira ya kumng'oa kiaina kwa kuchati hovyo ili asuse! Acha hizo buana!


15. ANKO Lao, binti miaka 28, kuna kijana niko katika uhusiano miaka miwili sasa na kaniahidi kunioa ila shida ni dini zetu, yeye Mwislamu nami Mkristo. Nifanyeje?

Editha Willy, Singida


Jibu: Kama mmechukuana kwa lengo la kupiga deiwaka, dini zinaweza kuwa vikwazo, lakini ukweli ishu za kidini hazijawahi kuwa kikwazo kwa wapendanao...kaeni chini mjadiliane ili mjue moja kuepuka kupotezeana muda. Kwani kama wenyewe mkiwa hamna maamuzi ni ngumu kushaurika!


16. ANKO Lao, binti miaka 21, shida yangu nilikuwa na mpenzi alinipa ujauzito kisha kuukataa siku nilipomjulisha na kibaya sikuwahi kujua kama alikuwa na mke. Nifanyeje?

Juliana Gregory, Kigoma


Jibu: Kiherehere gani kilichokufanya uneng'eneke kabla ya kuolewa? Hii ndio tabu yenu watoto wa 2000, hampigiwi mnacheza...mnavagaa hadi waume za watu. Ulichokitafuta umekipata, ila fanya uzungumze na jama'ako ujue atakusaidiaje, kwani ni kama tayari keshakuuzia kesi. Kazi kwako!


17. ANKO Lao, binti miaka 19 nina boy nampenda sana, ila tatizo kila nikimuomba pesa waka hajali kwa kudai hana wakati najua anazo. Nifanyeje?

Miriam Kasena, Dodoma


Jibu: Hilo ndilo tatizo lenu mabinti wa zama hizi...mkipendwa tu mnataka mpendwe na shida zenu kana kwamba hamna wazazi wa kuwahudumia! Huyo jama'ako ana haki ya kukuchunia na kama unaona pesa zinapatikana kirahisi, tafuta zako na wewe ili upunguze makasiriko! Wee vipi?!


18. ANKO Lao, binti miaka 19, kila mwanamume akinitokea huwa nampotezea kwa kumuona hanifai. Hii inatokana na kitu gani na nifanyeje nipate nitakayemuelewa?

Grace M.M, Moshi


Jibu: Kinachokusumbua kwa sasa ni akili za kitoto ulizonazo, pia ni bora uendelee hivyo hivyo kuwatolea mbavuni, kwani ukijichanganya tu wanaharibu fyucha yako...bado hujapevuka  kivile kwa ishu za malavidavi na unaonekana ni rahisi kuuvaa mkenge kwa mabazazi. Kuwa makini!


19. ANKO Lao, kijana miaka 26 kuna mwanamke ananipenda sana na tumeingia katika uhusiano, ila tatizo lake ana watoto wawili, akitaka nimuoe kabisa. Nifanyeje?

Andrea Mkuti, Moro


Jibu: Braza ukipenda boga, penda na ua lake...kama ulishamkubalia na kuliamsha, kipi kinakuzuia usimuoe? Iwapo kama analipa na sio mbibi jiachie tu! Kwa ishu ya watoto, dodosa ujue ni wa baba mmoja au la na wenyewe wapo wapi ili ujiweke salama dhidi ya kupigishwa shoti...si unajua kiporo huwa hakihitaji moto mkali, vilevile lazima ujue kitu gani kiliwafanya wamkache. Hivyo tu!


20. ANKO Lao, binti miaka 22, kuna mkaka tulikuwa tunapendana, lakini baada ya mwaka kabadilika ghafla na kibaya amehamia Dodoma, hata simu hanipigii nikimtumia meseji anauliza nani mwenzangu? Naumia sana kwani nampenda, nifanyeje?

Rachel Chipuza, Dar


Jibu: Alichokuwa anakitaka kutoka kwako ameshakipata ndo maana ameamua kukukaushia jumla, pia lazima ujue kuwa siku zote fimbo ya mbali huwa haiui nyoka! Acha kujitesa kwa mtu asiye na mpango nawe, huyo si mumeo, hivyo unapaswa kujiongeza maisha yaendelee! Wee vipi?