Prime
Huu ndo ukweli ndoa ya Esma Platnumz

Muktasari:
- Wakati Diamond akihusishwa kuingia kwenye ndoa na msanii wake wanaodaiwa kuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu, Zuchu huku kinachosubiriwa ni kama kweli wataoana, dada yake Esma stori zimesambaa ameachana na mume wake huku mwenyewe akiwamua kuweka wazi kuhusu hilo.
KWA sasa mitandaoni na vyombo vya habari stori ni ndoa za wasanii na wanamichezo kumeibuka tetesi zikimhusu dada wa nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Diamond Platnumz, Esma Platnumz ambaye alifunga ndoa na Jembe One, Februari mwaka jana.
Wakati Diamond akihusishwa kuingia kwenye ndoa na msanii wake wanaodaiwa kuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu, Zuchu huku kinachosubiriwa ni kama kweli wataoana, dada yake Esma stori zimesambaa ameachana na mume wake huku mwenyewe akiwamua kuweka wazi kuhusu hilo.
Esma ameliambia Mwanaspoti ndoa yake hiyo na meneja wa msanii Mvokali imekuwa ikichokonolewa na wadada wa mjini wanaomtaka mumewe, jambo linalochangia mgongano kati yao na kuweka wazi ndoa yao bado iko imara na anaendelea kutamba nayo.
Amesema habari hizo za kuambiwa ameachika zinatoka kwa maadui zake wenye kutaka uhuru uliopitiliza kwa mumewe na anawajua wanaomtakia mabaya.

"Sio Esma mimi niliyebadilika sasa kuanzia katika ndoa hadi maisha mengine ya mitandaoni, wacha watu waseme nimeachika, ila nakuambia ndoa bado ninayo na ninatamba nayo, ila wapo maadui wa ndoa yangu kwa majina nawajua wanaomsumbua mume wangu usiku kucha nashuhudia, wengine wanatuma jumbe fupi kikashani (inbox) hao wote ni wadada wa mjini wanaotaka utawala wa ndoa yangu," amesema Esma na kuongeza;
"Ndiyo hao hao wenye kutangaza nimeachika ili wapate kutumia uhuru wa kumtaka mume wangu, uzuri meseji zao nazisoma zote na nawaangalia tu. Kuna hao na wale wenye kufanya ushawishi wa kumtaka Jembe aniache bila sababu. Nawaambia bado nipo nipo sana ila salamu zao zimenifikia."

Wiki mbili sasa kumekuwa na habari kuhusu Esma kuamua kuikimbia ndoa ikielezwa sababu ni mume wake Jembe kumsaliti na ilidaiwa pia alidai talaka ili awe uhuru wa kuolewa na mwanaume mwingine atakayejitokeza.

Habari hizo zilikuwa gumzo ikidaiwa pia Esma hana bahati katika ndoa kwani kila ndoa atakayoolewa hadumu nayo hii ikiwa ni ya tatu baada ya kufunga ya kwanza na mwanamitandao Petit Man Septemba 20, 2014, kabla ya kuvunjika akiwa amepata mtoto wa kike na kuolewa tena Julai 2020 na mfanyabiashara Yahya Msizwa.