Harmorapa aja na wimbo wa Ramadhani

Tuesday May 04 2021
harmo pic
By Nasra Abdallah

Msanii wa muziki wa Bongofleva, Athuman Omary maarufu kwa jina la Harmorapa, ameachia wimbo wake mpya mahususi kwa ajili ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Wimbo huo ameupa jina la Yah Ramadhani, Harmorapa anausifia mwezi huo na kuhamasisha watu kufunga.

Pia anaelezea vitu gani mtu anapaswa kufanya ndani ya mwezi huo, ikiwemo kutoa sadaka na kufanya Ibada.

Katika wimbo huo Harmorapa amevaa kanzu na kilemba cha kichwani.

Akieleza kilichomsukuma kuimba, msanii huyo amesema ”Kwanza kabisa ni kutokana na kwamba watu tupo katika mwezi Mtukufu na pili mimi binafsi ni mtoto wa kiislam.

Wimbo huo anasema ameutengeneza kwa Bize Chechele na Good vibes studio.

Advertisement

Msanii huyu alijikuta akijizolea umaarufu miaka mitatu iliyopita na hii ni baada ya baadhi ya watu kumfananisha na msanii Harmonize.

Advertisement