Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Harmonize: Nilimpa dili Kajala

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Rajab Abdul maarufu Harmonize, amevunja ukimya kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wake na mrembo kutoka Bongo Movie, Masanja Kajala, huku akidai alikuwa akimpatia asilimia kumi ya kila alichoingiza wakati wakiwa pamoja.

Harmonize amesema ameamua  kuvunja ukimya huo, baada ya muda mrefu mrembo huyo kumuongelea mabaya kwa watu kuhusu yeye, huku akisahau mema ambayo alikuwa akimfanyia kipindi wapo pamoja.

Kupitia Instastory yake Harmonize aliandika: “Utaona walivyokuwa wakisubiri  muda niongee ili wajibu, nasisitiza mseme na mema sio kujichekesha.

“Simulia basi hapo kwenye TV kwamba nilikuwa nakupatia asilimia kumi ya kila ninachoingiza  kwenye show na ubalozi na namba zangu za siri za benki ulikuwa nazo,” alisema msanii huyo.

Harmonize aliongeza kuwa kwa bahati mbaya, bahati haiji mara mbili na Kajala hawezi kuja kuwa na furaha kiasi kile.

Aidha, alisema hilo halitawekezana ikiwa amevunja gari kutoka kwenye Range kurudi kwenye Toyota na kumwambia kuwa ni bora angempigia ili amsaidie hela ya matengenezo.

“Unajua mimi ni mzuri na ninapata hela, lia, saga meno, omba msamaha unaweza kufikiriwa ila njia unayotumia hutoboi, changanya na umri waacha tuone siongei,” alimaliza kuandika Harmonize.

Juhudi za kumpata Kajala kujibu hilo zilishindikana baada ya simu yake kutopatikana hewani.

Lakini kwa siku mbili mfululizo ambazo Harmonize amekuwa akiandika mambo mbalimbali kuhusu Kajala, Bongo movie huyo na bintiye Paula, walionekana na wakiwa wamerudishia video kwenye instastory wakionekana kucheka.