Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Harmonize, AY, Fid Q watemwa Grammy

Muktasari:

  • Tuzo hizo za 68 za Grammy zinatarajiwa kutolewa Februari 1, 2026 nchini Marekani na mastaa wa Bongo Fleva wakitemwa kwa mara nyingine katika kinyang’anyiro hicho.

NOVEMBA 7, 2025, waandaaji wa tuzo za Grammy waliachia listi ya majina ya watakaowania tuzo hizo kubwa duniani, kati ya majina hayo hakuna msanii wa Bongo Fleva hata mmoja.

Tuzo hizo za 68 za Grammy zinatarajiwa kutolewa Februari 1, 2026 nchini Marekani na mastaa wa Bongo Fleva wakitemwa kwa mara nyingine katika kinyang’anyiro hicho.

Kwa mujibu wa orodha ya uteuzi iliyotangazwa na ‘The Recording Academy’, vipengele vinavyohusu muziki wa Afrika vimeendelea kutawaliwa na mastaa kutoka Nigeria kama Burna Boy, Rema na Tyla wa Afrika Kusini.

Aidha msanii aliyeongoza kupata uteuzi mwingi zaidi ni Burna Boy ambaye ameteuliwa kuwania vipengele vitatu akifuatiwa na Rema (viwili) sawa na Tyla, huku Davido akiteuliwa katika kipengele kimoja cha ‘Best African Music Performance’.

Utakumbuka kuwa, nguli wa muziki wa Hip-Hop nchini, Fareed Kubanda maarufu Fid Q na Ambwene Yessayah (AY) waliandika historia mpya baada ya kuingizwa katika mchujo wa Tuzo za Grammy.

Kwa upande wa Fid Q, wimbo wake wa ‘Glory 2’ aliomshirikisha Damian Soul na Jose Chameleone ndio uliofanikisha hilo huku upande wa AY wimbo ‘Anganeka’ akiwa na Kanjiba na ule ‘Simuoni’ aliofanya na Harmonize ukiwa umemuingia kwenye mchujo huo.

Mbali na wasanii hao, naye mkali wa Bongo Fleva, Harmonize nyimbo zake nne zilifanikiwa kuingia katika hatua hiyo ya mchujo wa kuwania tuzo za Grammy, ambazo ni ‘Me Too’ ft Abigail Chams, ‘Simuoni’ aliyoshirikishwa na Ay, ‘Furaha’, na ‘Finally’ aliyomshirikisha Miri Ben-Ari, ziliwasilishwa katika kipengele cha ‘Best African Music Perfomance’.