Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hapa ndipo Hamisa Mobetto kawazidi kete Wema Sepetu, Nandy

Muktasari:

  • Hata hivyo, licha ya kutoupa nafasi kubwa muziki, bado kuna mengi ya kusimulia kuhusu Hamisa kwa yale ambayo amefanya hasa katika Bongo Fleva tangu akiwa video vixen hadi alipoamua kuwa mwimbaji. Fahamu zaidi. 

KWA miaka mingi jina la Hamisa Mobetto limekuwa juu katika tasnia ya burudani nchini akihusishwa na mitindo, muziki na filamu, fani ambazo ndio hasa chimbuko la umaarufu mkubwa alionao kwa sasa.

Hata hivyo, licha ya kutoupa nafasi kubwa muziki, bado kuna mengi ya kusimulia kuhusu Hamisa kwa yale ambayo amefanya hasa katika Bongo Fleva tangu akiwa video vixen hadi alipoamua kuwa mwimbaji. Fahamu zaidi. 


1. Hamisa ameshinda tuzo nyingi kupitia mitindo na urembo lakini katika muziki hajawahi kupata tuzo yoyote na hiyo ni sawa na ilivyokuwa kwa K-Lynn ambaye ni mshindi wa Miss Tanzania 2000, na mwimbaji wa zamani wa Tanzanites Band.


2. EP ya Hamisa, Your Truly (2022), imechanganya aina mbalimbali za muziki kama  Bongo Fleva, Baibuda, Afropop na Singeli, huku ikipita katika mikono ya watayarishaji muziki wakali kama S2kizzy, Abbah na Mocco Genius.

3. Hamisa aliandikiwa mistari yote aliyoimba katika wimbo wake, Sensema (2019) ambao alishirikiana na Whozu huku ukitayarishwa na S2kizzy wa Pluto Republic. Whozu ndiye aliyemwandikia lakini yeye si msanii wa kwanza kufanya hivyo kwa Hamisa, wapo wengine wengi tu waliotangulia kumwandikia mrembo huyo.


4. Mwanzilishi wa WCB Wasafi, Diamond Platnumz ndiye mwanamuziki pekee Bongo ambaye amefanikiwa kufanya video mbili za nyimbo zake na Hamisa. Wengine waliosalia kama Alikiba, Barnaba, Abdukiba, Quick Rocka n.k, wote wameshuti mara moja tu na mrembo huyo ambaye ni mshindi wa pili wa Miss Dar Indian Ocean 2011.


5. Baada ya kuusikia wimbo wa mwimbaji wa Singeli, Seneta Kilaka, Ex Wangu (2021), Hamisa alivutiwa nao na ndipo akamtafuta kupitia meneja wake ili warekodi remix yake. Kinachoshangaza ni kwamba remix hiyo ilikuja kufanya vizuri kuliko nyimbo zote walizowahi kutoa wawili hao na hadi sasa rekodi hiyo bado inasimamia.


6. Video ya wimbo, Ex Wangu Remix (2021), hadi sasa ndio namba moja kwa Hamisa na Seneta Kilaka kwa kufanya vizuri YouTube ambapo tayari imetazamwa (views) zaidi ya mara milioni 13.8.


7. Hamisa ana miaka zaidi ya minne bila kutoa wimbo mpya!, tangu alipoachia EP yake amekuwa kimya upande huo na huwenda ameachana na muziki kama alivyofanya katika uigizaji.

8. Video ya wimbo wa Alikiba, Dodo (2020) iliyosimamiwa na kampuni ya Rockshot, ndio ya mwisho kwa Hamisa kutokea kama video vixen, yaani baada ya hapo mrembo huyo ameipa kisogo kazi hiyo iliyoifanya kwa takribani miaka 10.


9. Hamisa ndiye msanii wa kike wa Bongofleva, mwigizaji na mwanamitindo kutokea Tanzania ambaye anaongoza kwa kuwa na wafuasi (followers) wengi zaidi katika mtandao wa Instagram akiwa nao milioni 12.2. Hamisa, Miss XXL, After School Bash 2010, amepata wafuasi hao baada ya kujiunga na mtandao huo wa kijamii hapo Desemba 2012 na ukurasa wake kuidhinishwa (verified) rasmi mnano Oktoba 2018.


10. Kwa jumla mastaa wa kike Bongo wanaomfutia Hamisa kwa kuwa na wafuasi wengi Instagram ni Wema Sepetu mwenye wafuasi milioni 11.6, Shilole mwenye wafuasi milioni 10.8, na kisha Nandy mwenye wafuasi milioni 10.6.