Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hamisa avunja ukimya, afunguka ishu ya ujauzito

MOBETTO Pict

Muktasari:

  • Februari 16, 2025 Hamisa Mobetto na Aziz KI walifunga ndoa kwenye msikiti wa Mbweni jijini Dar es Salaam.

“LISEMWALO lipo na kama halipo laja, kwani sina haki ya kubeba ujauzito jamani? Tena nafurahia kumzalia Aziz KI mume wangu wa ndoa.” Haya ni maneno ya mrembo Hamisa Mobetto ambaye ni mke wa nyota wa zamani wa Yanga na kwa sasa anakipiga Wydad AC, Stephanie Aziz KI.

Kama hujui hili, basi jua kupitia Mwanaspoti kuwa, habari ya mjini kwasasa ni Hamisa anadaiwa kunasa ujauzito hivyo yupo mbioni kutimiza ndoto yake ya kupata mtoto wa tatu hivi karibuni.

Hamisa ameibua gumzo mitandaoni kufuatia muonekano wake wa sasa, baada ya kutupia picha mtandaoni ambayo iliwafanya wajuzi wa mambo kuikagua vilivyo na kuhitimisha kuwa ni mjamzito.

Mwanaspoti lilimsaka ili kuthibitisha madai hayo ambapo amesema kama ni kweli hakuna tatizo lolote yeye kupata ujauzito.

“Jamani habari nyingine ni njema sana, kama kuna mtu amewaambia basi siyo mbaya maana nipo huru kuwa mjamzito kwani sijasababisha chochote kibaya kwa mtu, na kama ni kweli nafurahia kuzaa na mume wangu.”

Mwanadada huyo amewatoa hofu watu ambao wanamwambia kuwa ni mjamzito kwa kuwaambia, suala la mimba halijifichi kwani kama ipo haiwezi kujificha kwa sababu mimba hainywei bali inakua siku hadi siku hivyo wawe wapole tu mpaka muda utakapofika itaonekana bila kificho au kama ni mtoto, watamuona.

Februari 16, 2025 Hamisa Mobetto na Aziz KI walifunga ndoa kwenye msikiti wa Mbweni jijini Dar es Salaam.