Halima Kopwe Miss Tanzania 2022

Saturday May 21 2022
Miss PIC
By Nasra Abdallah

Dar es Salaam. Hatimaye fainali za kumsaka Miss Tanzania 2022 zimefika tamati, na taji kwenda kwa aliyekuwa Miss Mtwara,Halima Kopwe.

Halima ametangazwa usiku wa jana Mei 20,2020 katika fainali za mashindano hayo zilizofanyika ukumbi wa Mlimani City.

Miss huyo ameondoka na gari aina ya Mecedez Benzi yenye thamani ya Sh40 milioni na kitita cha Sh10 milioni.

Katika mashindano hayo, Halima aliwabwaga warembo 20 aliopanda nao jukwaani kuchuana na hivyo kukata tiketi ya kwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya dunia.

Nafasi ya pili  katika mashindano hayo ilienda kwa Angel Alfred aliyeondoka na Sh5 milioni, huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na  kwa Otaiga Mwema aliyezwadiwa Sh3 milioni.

Halima anakuwa Miss wa nne tangu mashindano hayo yalipoanza kuratibiwa na kampuni ya 'The Look', tangu mwaka 2018 ambapo mshindi wa mwaka huo alikuwa Queen Elizabeth Makune, mwaka 2019 akawa Sylvia Sebastian na mwaka 2020 alikuwa Rosemary Manfere.

Advertisement
Advertisement