Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gari lililobeba mwili wa Ally Star  laharibika njiani, mazishi kufanyika leo

GARI Pict

Muktasari:

  • Msafara huo uliondoka Dar es Salaam jana saa saba mchana ukiwa umebeba mwili wa marehemu kwa ajili ya mazishi yaliyopangwa kufanyika jioni. Hata hivyo, safari ilikumbwa na vikwazo vilivyosababisha ratiba hiyo kubadilika.

Mwili wa mtunzi, mwimbaji na mpiga gitaa, Ally Star unatarajiwa kuzikwa leo asubuhi wilayani  Kilosa, mkoani Morogoro, baada ya msafara ulioubeba kutoka Dar es Salaam kuchelewa kufika kufuatia changamoto zilizojitokeza njiani.

Msafara huo uliondoka Dar es Salaam jana saa saba mchana ukiwa umebeba mwili wa marehemu kwa ajili ya mazishi yaliyopangwa kufanyika jioni. Hata hivyo, safari ilikumbwa na vikwazo vilivyosababisha ratiba hiyo kubadilika.

Mwandishi wa Mwanaspoti aliyekuwa miongoni mwa wasafiri katika msafara huo alishuhudia gari lililobeba jeneza la Ally Star likiharibika eneo la Msolwa, hali iliyosababisha msafara kusimama kwa takribani saa mbili kabla ya tatizo hilo kurekebishwa.

Baada ya gari hilo kupona waombolezaji waliokuwa katika msafara walifanya dua kabla ya kuendelea na safari.

Ilipofika saa 3.45 usiku eneo la Dakawa gari likiharibika kwa tali la nyuma upande wa kushoto kupasuka.

Awali, familia ilikuwa imepanga kufanya mazishi usiku huo huo, ambapo hata kaburi lilikuwa tayari limeshachimbwa tangu mchana, lakini kutokana na kuchelewa kwa msafara na ushauri uliotolewa iliamuliwa kuwa mazishi yafanyike asubuhi, 

Akizungumza na Mwanaspoti, mdogo wa marehemu, Salehe Hemed amesema, "mazishi ya Ally Star yatafanyika saa mbili asubuhi karibu na nyumbani  katika eneo ambalo pia ndiko yalipo makaburi ya familia."