Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fursa tamu zitakazomfuata Mobetto

MOBETTO Pict

Muktasari:

  • Hisia za furaha ni baada ya kusikia nyota huyo atacheza michuano ya Kombe la Dunia la Klabu na hata kama hataanza kwenye kikosi cha Wydad, lakini atakuwa sehemu la benchi kukipiga dhidi ya Manchester City.

USAJILI wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga na timu ya taifa ya Burkina Faso, Stephanie Aziz Ki kwenda Wydad Casablanca ya Morocco hivi karibuni na hatimaye kwenda kupiga katika fainali za Kombe la Dunia la Klabu nchini Marekani kumeibua hisia tofauti ndani na nje ya uwanja wa soka.

Hisia za furaha ni baada ya kusikia nyota huyo atacheza michuano ya Kombe la Dunia la Klabu na hata kama hataanza kwenye kikosi cha Wydad, lakini atakuwa sehemu la benchi kukipiga dhidi ya Manchester City.

Hisia nyingine ni huzuni, mbali na kufurahia mafanikio, lakini  nyota huyo kipenzi cha mashabiki wa Yanga atabaki mioyoni mwa Watanzania kutokana na kile alichofanya ndani ya misimu miwili nchini Tanzania.

Nje ya soka, lakini habari hii pia imevutia mashabiki wa burudani, hasa kutokana na Aziz Ki kumuoa mrembo wa Kitanzania Hamisa Mobetto ambaye ni miongoni mwa watu maarufu nchini.

Hamisa ambaye ni mwanamitindo, mfanyabiashara na msanii wa muziki, amekuwa akifuatiliwa na mashabiki na kuongeza wafuasi  kutokana na wawili hao kuwa mwili mmoja sasa.

Wakati Aziz KI akipata fursa nyingine kwenye maisha yake ya soka akisaini mojawapo ya klabu kubwa Afrika, nafasi hiyo pia inaweza kuibua fursa mpya za kimaisha, kibiashara na kijamii kwa Mobetto.

Ingawa usajili wa KI kwenda Wydad ni habari kubwa kwa upande wa michezo, Hamisa anaweza kunufaika kwa kutumia umaarufu wa mumewe kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii na fursa za kibiashara hasa kama atacheza karata zake vizuri kwa kujijengea ushawishi kimataifa.

Mwanaspoti inaamini kwamba hatua ya Aziz Ki kusajiliwa na Wydad inaweza kuwa na manufaa kwa Mobetto kutoka kuongezeka kwa umaarufu wake kimataifa hadi kufunguka kwa milango ya fursa mpya nje ya mipaka ya Tanzania.


KUONGEZA UMAARUFU

Kabla ya kuwa na uhusiano na kufunga ndoa na Aziz KI, tayari Mobetto alikuwa na umaarufu nchini kupitia kazi zake za sanaa ya uigizaji na kuimba, lakini pia kwenye biashara za nguo.

Ndoa hiyo itamnufaisha Mobetto na kuongeza pia ufuatiliwaji wake kimataifa, hasa katika ukanda wa Afrika Kaskazini na Mashariki. Na kwa Aziz KI kuchezea timu kubwa ya Wydad, mojawapo ya klabu yenye mafanikio makubwa na maarufu Afrika kunaweza kuongeza umaarufu wa Mobetto zaidi na kupata ufuasi mkubwa zaidi kimataifa.

Mbali na Aziz, lakini klabu hiyo inamiliki wachezaji kutoka mataifa mbalimbali duniani hivyo mlimbwende huyo atapata nafasi ya kushiriki matukio au maisha ya kifahari yanayohusiana na soka la kimataifa.


BIASHARA

Umaarufu huo unaokuja unaweza kumletea Mobetto dili zaidi za kibiashara, hasa kwa chapa (brand) zinazolenga soko la Afrika kupitia mumewe.

Mobetto keshapata na ataendelea kunasa fursa za kwenda Morocco au nchi nyingine kupitia matukio yanayomhusisha Aziz kama vile mechi kubwa au hafla za timu yake na hii itamwezesha kujenga mtandao wa kimataifa.

Mwanamitindo huyo anaweza kutumia uhusiano wao kama sehemu ya chapa kupata dili zaidi za matangazo (endorsements). Wadhamini na kampuni hupenda kutangaza kupitia watu maarufu wenye mvuto wa kimataifa, hivyo mrembo huyo anaweza kupata ubalozi wa bidhaa za urembo na mitindo.

Mwanadada huyo pia anaweza kushirikiana na wazalishaji wa bidhaa zinazolenga masoko ya Morocco au Mashariki na Kaskazini mwa Afrika, akitumia jina la mumewe - Aziz KI kama kichocheo.


KUKUZA CHAPA

Mobetto ni mwanamitindo na mfanyabiashara, umaarufu wa mpenzi wake ukipanda anaweza kutumia fursa ya kushirikiana na chapa mbalimbali za nguo au vipodozi kutoka Morocco au nchi zingine ikiwamo kuuza nguo zake maarufu 'Mobetto Styles' na umaarufu huo pia unaweza kumuwezesha kufungua masoko nchi kama Algeria, Misri na nyinginezo.