Flora amepigwa komeo kabisa

BINTI mwenye mvuto na anayefanya vizuri kwenye filamu za Bongo, Flora Mvungi hivi karibuni alivishwa pete ya uchumba na Hamis Baba ëH. Baba. Tukio hilo la aina yake lilifanyika katika Hoteli ya Atriums, Sinza na kuhudhuriwa na marafiki wa karibu. ìFlora kwangu ni mke mwema ndio maana nimekuwepo naye kwa muda mrefu na leo hii tupo katika moja ya hatua ya kuutambulisha umma kwa vitendo kuwa sisi ni wachumba kwa vitendo na katika tukio hilo la pete ndio alama kubwa sana kwetu na ishara ya upendo tulio nao katika uhusiano wetu,îalisema H. Baba. Wasanii hawa wamekuwa katika hali ya uhusiano kwa muda mrefu huku uhusiano wao ukikumbwa na mikasa ya hapa na pale hadi sasa wameweza kuvalishana pete ya uchumba. Naye Frola hakuwa na la kusema zaidi ya kufurahia tukio ambalo amesema amejenga historia katika maisha yake.