Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chino kurudi shule, amtaja mzungu

CHINO Pict

Muktasari:

  • Chino ambaye anapendelea kuimba mtindo wa Amapiano, alisema anaamini baada ya kutimiza ndoto yake ya kurudi shule, mambo mengi yatakuwa mazuri kwani hata muziki wake utazidi kufika kimataifa ikiwa ni pamoja na kuimba nyimbo ambazo zinaweza kuinua uchumi wa Taifa.

Msanii wa Bongo Fleva, Chino Kidd amesema pamoja na umaarufu wake anahitaji sana kurudi shule ili aongeze uwezo wake wa kuimba.

Chino ambaye anapendelea kuimba mtindo wa Amapiano, alisema anaamini baada ya kutimiza ndoto yake ya kurudi shule, mambo mengi yatakuwa mazuri kwani hata muziki wake utazidi kufika kimataifa ikiwa ni pamoja na kuimba nyimbo ambazo zinaweza kuinua uchumi wa Taifa.

"Mimi shule lazima nirudi tu,  kwani kule ndo kwenye mipango na maisha mazuri, naelewa bila shule mambo mengi tunakuwa tunafanya lakini tunakosea, mashabiki wangu ambao wanatamani kuniona nikirudi shule wanaamini nitafanya hivyo kwa ajili ya kuongeza uwezo wa kazi yangu," alisema Chino.

Alisema pia kwa sasa ameanza kujua lugha ya Kiingereza kidogo na ujuzi huo amepata kwa mpenzi wake mzungu.

"Sasa hivi nimeshaanza kuifahamu lugha ya Kiingereza, natamani sana kuifahamu kuongea zaidi, mpenzi wangu mzungu anajitihida kubwa sana kunifundisha, japo watu wameanza kuzusha nimeachana nae. Mimi ni mwehu niachane na mwalimu wangu wa lugha? bado nipo naye na ninatamba naye," alisema Chino.