Billnass afunguka kutoka na Yammy

Muktasari:
- Billinas aliliambia mwanaspoti yeye sio sababu ya Yammy kutoka kwenye lebo hiyo na watu wanatakiwa wamheshimu kwenye hili.
MSANII wa Bongo Fleva, Billnass amesema watu waache kupotosha kwa kudai yeye ndiyo sababu ya Yammy aliyekuwa chini ya lebo ya The African princess inayomilikiwa na Nandy.
Billinas aliliambia mwanaspoti yeye sio sababu ya Yammy kutoka kwenye lebo hiyo na watu wanatakiwa wamheshimu kwenye hili.
"Sijajua ni mpuuzi gani mmoja ambaye ameanzisha hizi habari za kunichafua mimi, yaani inabidi watu waniheshimu sana kwenye hizi mambo, sina ujinga huo na wala sijawahi kufanya hivyo na yule binti tunaheshimiana sana, watu waache kupotosha maneno maneno.
"Wapo wanaosema mke wangu Nandy ananitetea kwenye hili, yaani siyo ananitetea, bali anaona vitu vinavyotengenezwa ni vya kitoto na hasa kutuharibia tu kwenye ndoa yetu kupitia doa. Kwanza Yammy tunamfahamu mpenzi wake na wala hatuna shaka naye, ameondoka kwa vizuri hana mgogoro wowote na mke wangu wala mimi, ifike hatua watu tuheshimiane jamani," alisema Billnass.