Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BONGO MUSIC FACTS: Miaka saba ya Lava Lava WCB Wasafi bila tuzo

Muktasari:

  • Akiwa ni msanii wa tano kusainiwa na WCB Wasafi, rekodi lebo yake Dimaond Platnumz, Lava Lava ametoa EP moja, Promise (2021) huku nyimbo zake zikiwa na mamilioni ya wasikilizaji mtandaoni. Fahamu zaidi.

UKITAZAMA namba zake katika majukwaa ya kusikiliza muziki, Lava Lava ni msanii mkubwa ila hapewi heshima anayostahili pengine kutokana na wenzake wa WCB Wasafi wanavyofanya vizuri zaidi yake.

Akiwa ni msanii wa tano kusainiwa na WCB Wasafi, rekodi lebo yake Dimaond Platnumz, Lava Lava ametoa EP moja, Promise (2021) huku nyimbo zake zikiwa na mamilioni ya wasikilizaji mtandaoni. Fahamu zaidi.


1. Kabla ya kuwa mpigapicha wa Diamond Platummz, Lukamba aliwahi kufanya kazi ya utayarishaji muziki na miongoni mwa wasanii aliowahi kurekodi kazi zao ni pamoja na Lava Lava ambaye wakati huo bado alikuwa hajasainiwa na WCB Wasafi.


2. Hapo awali Lava Lava aliwahi kujifunza uimbaji chini ya Tanzania House of Talent (THT), lakini hakufanikiwa kutolewa na taasisi hiyo ambayo Diamond naye aliwahi kuomba nafasi hapo ila akakosa.


3. Tangu amejiunga na WCB Wasafi hapo Mei 2017,  Lava Lava hajashinda tuzo yoyote katika muziki akiwa ni sawa na Rich Mavoko, Queen Darleen na D Voice ambao nao hawajashinda tuzo chini ya rekodi lebo hiyo. Wasanii wengine wameshinda tuzo mbalimbali tena za kimataifa mathalan Harmonize (AFRIMMA), Rayvanny (BET), Zuchu (AFRIMMA) na Mbosso (HiPipo). 


4. Lava Lava aliachia wimbo wake, Wanga (2020) akiwa na Meja Kunta bila ruhusa ya uongozi wake na huo ndio wimbo wa kwanza wa singeli kuachiwa chini ya WCB Wasafi, kisha ukafuata Miss Buza (2020) wa Rayvanny.


5. Harrier ndio gari la kwanza kwa Lava Lava kupewa na WCB Wasafi ingawa gari ya ndoto zake ilikuwa ni Crown. Na Rayvanny gari lake la kwanza kupewa lilikuwa ni Rav4 , Harmonize - Mark X, Mbosso - Harrier na Zuchu - Vanguard.


6. Lava Lava ni msanii wa sita Tanzania kufikisha wafuatiliaji (subscribers) zaidi milioni moja katika mtandao wa YouTube. Waliomtangulia ni Diamond Platnumz, Rayvanny, Harmonize, Mbosso na Zuchu. Na baada ya Lava Lava waliofuatia ni Alikiba, Nandy, Marioo, Aslay, Rose Muhando, Jux na Jay Melody, hivyo kuifanya Tanzania kuwa na wasanii 13 wenye ‘subscribers’ zaidi ya milioni moja YouTube ikiwa ni nchi pekee Afrika Mashariki na Kati yenye rekodi hiyo.


7. Kabla ya kutambulishwa Lava Lava alikuwa sehemu ya bendi ya Diamond, baada ya kuzunguka naye kwenye shoo nyingi Chibu akaona kijana ameivaa kuingia katika muziki.


8. Wimbo wa Shilole, Nyanganyanga (2015) ameandikiwa na Lava Lava ambaye alifanya hivyo kama zawadi kwake kwani Shishi ndio staa wa kwanza Bongo kuwa naye karibu hapo awali.


9. Video ya wimbo wake wa kwanza kuachia chini ya WCB Wasafi, Tuachane (2017) hadi sasa ndio iliyotazamwa zaidi YouTube ikiwa na ‘views’ zaidi ya milioni 22 na Lava Lava ndio msanii pekee wa Wasafi mwenye rekodi hiyo.


10. Kipindi Rich Mavoko akiwa WCB Wasafi alimpa Lava Lava mdundo wa wimbo wake, Rudi (2017) ili aingize sauti ila Lava Lava akaona haendani nao, ndipo Mavoko akarekodi na kumshirikisha Patoranking kutokea Nigeria na ni moja ya nyimbo za Mavoko zilizofanya vizuri.