Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bi Mwenda anusurika kupigwa

MWENDA Pict

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti, Bi Mwenda alisema kuna siku alitaka kupigwa  na watu maeneo ya Tandika Sokoni, kisa tu kufikisha kwake ujumbe kupitia sanaa wakidhani ni kweli mchawi.

MWIGIZAJI mkongwe wa filamu, Fatuma Makongoro ‘Bi Mwenda’ amesema ameacha kuigiza nafasi za ‘kichawi’ baada mashabiki zake kumhisi ni mchawi kweli.

Akizungumza na Mwanaspoti, Bi Mwenda alisema kuna siku alitaka kupigwa  na watu maeneo ya Tandika Sokoni, kisa tu kufikisha kwake ujumbe kupitia sanaa wakidhani ni kweli mchawi.

“Najua kazi nimeifanya ya kufikisha ujumbe kwenye vipengele vya kucheza mwanamke mchawi, lakini nimeona niachane navyo kwa sasa, kwa umri wangu  unavyozidi kwenda mashabiki zangu wananihisi kweli mimi ni mchawi. Nilishawahi kutaka kupigwa sokoni Tandika kwa kudhaniwa ni mchawi nafanya chuma ulete kwenye biashara za watu, aisee sitaki tena hiyo nafasi,” alisema Bi Mwenda.

Bi Mwenda ambaye alianza  sanaa ya uigizaji mwaka 1998  aliendelea kusema, tangu hapo ikawa imewaletea ugumu waongozaji kumpa nafasi ya kucheza lakini pia ndio chanzo cha kutovuma kwa sasa.

“Sidhani kama kukataa kucheza nafasi ya uchawi ndio chanzo cha mimi kutosikika kwa sasa, bali ni upepo tu ambao umekuwa ukichukua vipaji vya waigizaji kila wakati, lakini mimi director yeyote akinihitaji kufanya kazi nipo tayari lakini sio nafasi ya uchawi.”

Bi Mwenda aliwahi kutamba katika Kundi la Kaole lililokuwa na wasanii kama vile marehemu Steven Kanumba, Vincent Kigosi ‘Ray’, Muhogo Mchungu, Kipemba, Dk. Cheni, Mtunisi, Frank, Nina, Nana, Norah, Kibakuli, Nyamayao,  marehemu Max, Zembwela, Bambo, Kingwendu, Swebe, Zawadi na wengine wengi.

Kwa sasa mkongwe huyo anatamba na tamthilia kadhaa ikiwamo ya Huba akiwa na baadhi ya mastaa wenye damu changa na wazoefu kama yeye akiwamo, Muhogo Mchungu.