Babu Tale adai Basata, Cosota ni wababe wa wasanii siyo watoa elimu

Monday June 06 2022
tale pic
By Habel Chidawali

Dodoma. Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) na Chama cha Hakimiliki Tanzania (Cosota) wametupiwa lawama kwamba hawana msaada wowote kwa wasanii badala yake wamekuwa ni maadui.

Shutuma hizo zimetolewa leo Juni 6, 2022 bungeni na Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Hamisi Taletale maarufu Babu Tale wakati akichangia hotuba ya makadilio ya mapato na matumizi kwa Wizara ya Sanaa, Tamaduni  na Michezo kwa mwaka 2022/23.

“Basata imekuwa ni polisi, hawatoi elimu kwa wasanii badala yake wanasubiri kuwafungia wasanii pale wanapokosea, kila wakati wanawaza kuwafungia na wamekaa kwa kutegeshea,” amesema Taletale.

Mbunge huyo amesema baadhi ya watumishi katika Wizara ya Michezo wana alichokiita roho mbaya zaidi hawafikirii kuwapeleka wasanii mbele ila wamejigeuza kuwa polisi.

Kuhusu Cosota amesema wakipelekwa Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa (Takukuru) itawafunga wote kutokana na mazingira ya harufu ya rushwa kwenye kitengo hicho.

Amesema Cosota ni gari bovu ambalo haliangalii uwezo wa mtu katika Sanaa badala yake wanatoa fedha za gawio bila kwa watu kwa majina siyo kwa kuangalia uwezo na mchango wao waliouonyesha.

Advertisement
Advertisement