Baba Levo awaamsha Yanga kwa Mkapa

Sunday August 29 2021
baba pic
By Ramadhan Elias

MSANII wa Muziki wa kizazi kipya Baba Levo amewaamsha  kwa nyimbo mashabiki wa Yanga waliopo ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa kwenye kilele cha tamasha la Wiki ya Mwananchi.

Baba Levo aliingia uwanjani sa 9:30 mchana dakika chache baada ya mechi kati ya Yanga Princess na Ilala Queens kumalizika na kuanza kuimba nyimbo zake ambazo mashabiki walionekana kuzikubali na kuinuka kucheza.

Baba Levo aliingia na madansa watatu na kanza kwa nyimbo yake iitwayo ‘Kamseleleko’ na mashabiki waliopo uwanjani hapo kuamsha shangwe la kufa mtu.

Baada ya nyimbo hiyo, Baba levo alipiga nyimbo nyingine iitwayo Amapiano kisha kuondoka uwanjani hapo huku mashabiki wakiendelea kumshangilia.

Advertisement