Aunty aipotezea ‘Leo’ ya Kusah, Ruby

New Content Item (3)
New Content Item (3)

KAMA unadhani msanii wa filamu Bongo, Aunty Ezekiel amekerwa au kuchukizwa na ujio wa kolabo ya wimbo ‘Leo’ ulioimbwa na wanamuziki Kusah na Ruby, basi hautakuwa sahihi.

Akizungumza na Mwanaspoti, Aunt Ezekiel amesema anachoangalia ni familia yake kuwa na amani na upendo, na hataki kufunguka mambo ya watu wengine kwani hana huo muda.

Ruby ameachia wimbo mpya uitwao Leo ambao amefanya na mzazi mwenzake Aunty Ezekiel, Kusah.

“Kwa sasa niko bize kidogo, ila hilo swali lako la kuhusu Kusah kufanya kolabo ya wimbo na Ruby mimi ninachoangalia ndani kwangu kama kuna amani na upendo siwezi kuwazungumzia watu wengine, ila siku nikiamua kufunguka basi nitafunguka, lakini kwa sasa sina muda huo,” alisema Aunt Ezekiel.

Ruby na  Kusah walikuwa hawaelewani hadi kusemana vibaya kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii, halikadhalika Ruby na Aunt Ezekiel pia siku chache zilizopita walitupiana maneno kwenye mitandao.

Ujio wa ngoma hiyo imekuwa gumzo kila kona kwa kile tu Ruby baada ya kufanikiwa kupata mtoto na Kusah hawakuchukua muda kwenye mahusiano yao wakaachana, ndipo Kusah akaanzisha mahusiano mapya na Aunt Ezekiel na kufanikiwa kupata mtoto na hadi sasa wanaishi pamoja.

Hii ni kolabo ya tatu Kusah na Ruby kufanya, ya kwanza ni ile ya wimbo wa ‘Kelele’, pili ‘Nadondosha’ na ya tatu ni ‘Leo’ zote zinafanya vizuri hadi sasa katika anga ya muziki wa Bongo Fleva. Kwa sasa Aunty Ezekiel anafanya shughuli zake za uigizaji na biashara, huku akiwa miongoni mwa wasanii na walimbwende wakongwe katika tasnia ya urembo nchini.