Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Anko Lao... Majibu Konkii

Muktasari:

  • Jibu: Hicho unachokifanya sasa kitakugharimu, pale jamaa atakapokata tamaa na kujiongeza kwa kusaka chaka jingine, ilihali kumbe nawe unamzimia kichizi. Cha kufanya jiachie maisha yaendelee.

1. ANKO Lao, binti miaka 20 kuna kijana ananipenda sana, lakini akinifuata najifanya sitaki ujinga wake, ila ukweli mie mwenyewe nampenda kinoma hadi naumwa, japo sijamwambia. Nifanyeje? 
Nayla Mfaume, Ilala


Jibu: Hicho unachokifanya sasa kitakugharimu, pale jamaa atakapokata tamaa na kujiongeza kwa kusaka chaka jingine, ilihali kumbe nawe unamzimia kichizi. Cha kufanya jiachie maisha yaendelee.

2. ANKO Lao, mie ni binti niliyezalishwa na mtu niliyempenda, lakini akanitema yupo mkoani na mwanamke mwingine, nimekuwa nashindwa kufanya maamuzi kwa sasa nikiamini atarudi tuendelee kumlea mtoto, kiasi nawatema wanaotaka kunioa. Nifanyeje?
C. B. James, Moro

Jibu: Ulibugi sana kukubali kuzalishwa kabla ya ndoa na kuendelea kumuamini eti jamaa atarudi kwako wakati hana taimu nawe...Cha kufanya ni kukubali huyo hakuwa riziki yako, kisha mtoe kichwani na kuendelea na yako ukitafuta muaminifu akuoe nawe maisha yaendelee. Hivyo tu!

3. ANKO Lao, kijana miaka 31 kuna binti nampenda sana na nimeshamueleza nia yako kwako nikitaka kumuoa kabisa, lakini ananiletea mashauzi mengi, kiasi huwa naumia sana. Nifanyeje?
John Cena, TMK

Jibu: Ukiona hivyo, ujue bibie ana mtu wake ndo maana anakuletea miyeyusho, lakini kwa vile vijana wa zama hizi huwa hamjiongezi, unaendelea kumbembeleza kama unaombaa kazi. Jiongeze tafuta pisi nyingine kali kisha uoe. Kuendelea kulazimisha malavidavi utajiumiza bure. Wee vipi?

4. ANKO Lao, kijana miaka 26 kuna mdada nampenda naye anaonekana kunipenda kwa viasharia anavyonionyesha, ila nashindwa kumwambia kwani naheshimiana naye sana. Nifanyeje nimnase?
Pakwale P, Mikumi Moro

Jibu: Buana wee si useme tu una domo zege, ishu za kuheshimiana ndo nini wakati umeshaona dalili zote za bibie anakuzimia? Kama upo siriazi na unamuelewa huyo manzi jilipue tu, kwani unaweza kuzubaa wajanja wakaruka naye kisha ukaishia kusononeka kiboya... Hivyo tu!

5. ANKO Lao, kijana miaka 24, nina mpenzi tunapendana, ila tatizo mgumu sana kuachia mzigo, licha ya kula vyangu. Nikimlazimisha hutoa maneno makali na kudai tuachane, nami sipo tayari. Nifanyeje?
Festo Fidel, Kagera

Jibu: Huyo bibie keshakuona wewe duwanzi ndo maana anakupelekesha atakavyo, akiendelea kukulia vyako na kuishia kukusaundisha. Kama umemzimia sana, peleka posa kwao uoe ili ujipakulie minyama, la tafuta pisi nyingine maisha yaendelee kwani kwa bibie huyo utaishia kula kwa macho tu. Shauri yako!

6. ANKO Lao, kijana miaka 20 kwa miaka sita sasa sina mpenzi na wala sijawahi kupiga shoo, je naweza kupata tatizo?
Frank, Kigamboni

Jibu: Kwa umri ulionao ni wazi wewe ni wale wenye midomo zege isiyoweza kuimbisha na kuishia kupiga puchu...Kutokuwa na mpenzi ama kutopiga shoo hakuna madhara, ila kupiga puchu kunazingua na kwa taarifa yako ukiendekeza huo uduwazi ujue kabisa utaishia kuwa nyoka wa kibisa. Kazi kwako!

7. ANKO Lao, binti miaka 20, kuna boy nampenda sana naye ananipenda, ila tatizo lake ana mademu wengi na huwa haniamini kabisa sasa. Nifanyeje?
Piurity Rayan

Jibu: Kama umegundua jamaa ana macho miamia wee wa kazi gani au unataka kupewa vijidudu? Kubali matokeo kwa kujituliza kwenu ajitokeze mtu wa kuja kukuoa maisha yaendelee. Hivyo tu!

8. ANKO Lao, nina miaka 34 ni mama wa watoto wawili, niliozalishwa tu na kwa sasa natamani kupata mume, lakini nimeathirika. Nitapata vipi wa kunipenda na kunioa, nifanyeje?
Salome, Mbeya

Jibu: Pole sana kwa changamoto uliyonayo, hata hivyo hupaswi kukata tamaa, kwani VVU kwa sasa vinadhibitiwa na kama umeanza kliniki ya ARV, naamini unaweza kupata mwenza hasa kama utajiweka wazi. Maisha ataendelea hata kama umeungua tofauti na ilivyokuwa zamani. Hivyo tu!

9. ANKO Lao, miaka 27 nina mchumba amenipangia chumba na kunipa mtaji wa biashara na ananipenda sana, shida ni kwamba ni mume wa mtu. Nifanyeje?
Happy Kanka, Dar

Jibu: Hakuna uchumba na mume wa mtu, sema wewe ni kivuruge uliyekosa aibu kwa kudandia vya watu...kwa umri ulionao ungejituliza ungepata kabisa mtu wako wa kukuoa kabisa kuanzisha familia kuliko hicho unachokifanya, kwani mwenye mali akikushtukia utajuta kuzaliwa. Shauri yako!

10. ANKO Lao, binti miaka 20 ni mtu wangu ninampenda sana, ila tumegombana, naomba ushauri.
Stella

Jibu: Aliyekuambia mie mjumbe wa nyumba 10 nani hadi uniletee kesi yenu ya kugombana? Halafu kwa umri ulionao, ni vyema ungekomaa kuitafuta kesho yako kuliko kujibebisha kwa hiyo njemba isiyokuzimia...usipojiangalia utakuja kung’olewa meno, kwani anayekuzimia hawezi akakuzingua.