Cheka atakiwa kupunguza kilo mbili, kuzichapa Kesho Morogoro

Muktasari:

Cheka atazichapa na Kaoneka bondia pekee aliyewahi kumchapa Hassan Mwakinyo kwa Knock Out (KO) pambano la raundi 10.


Bondia Francis Cheka amelazimika kukata uzito kwa kupunguza kilogramu mbili ili kufikia uzani wa super middle anatokaiwa kupigania kwenye pambano lake la kesho Ijumaa.

Cheka atazichapa na Shaban Kaoneka kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, pambano ambalo litakuwa la kwanza kwa bondia huyo kuonekana ulingoni baada ya lile ya Desemba 26, 2018 alipochapwa kwa Knock Out (KO) na Abdallah Pazi (Dullah Mbabe).

Cheka na Kaoneka wamepima uzito na afya tayari kupanda ulingoni kuzichapa pambano lisilokuwa la ubingwa la raundi 10 la uzani wa super middle.

"Nimelazimika kupunguza kilo 2 ili nicheze pambano hilo ambalo tutapigania uzani wa kilogramu 78," amesema bondia huyo bingwa wa zamani wa dunia wa WBF.

Amesema amefanikiwa kwa kufanya mazoezi makali ya kukimbi kwenye mashine na kuwaahidi mashabiki wake kumshuhudia kivingine ulingoni kesho.

Amesbainisha kwamba mashabiki wake ndiyo wataamua kama anastahili kuendelea au astaafu baada ya kupima uwezo wake kwenye pambano la kesho.

"Kama nitafanya vizuri, baadae mwaka huu nitapigana pambano la ubingwa na bondia kutoka Cameroon, hivyo kwenye pambano na Kaoneka mashabiki ndiyo wataamua kama kiwango changu kinaridhisha niendelee au vinginevyo," amesema Cheka akisisitiza

"Niko vizuri, sijarudi ulingoni kwa bahati mbaya, japo ile kasi ya mwanzo itapungua, lakini ufundi na uzoefu ninavyo vya kutosha.

Pambano la Cheka na Kaoneka litaanza saa 9 Alasiri na linatarajiwa kumalizika saa 12 jioni likitanguliwa na mengine matano huku Kaonekana akimtahadharisha Cheka kwa kumpa angalizo kuwa asitarajie mteremko kesho.