#WC2018: Kombe la Dunia latajirisha wajanja China

Friday July 13 2018

 

Beijing, China. Fainali za Kombe la Dunia 2018, zinazoendelea nchini Russia, zimewatajirisha wezi walioamua kutumia udhaifu na mashabiki wengi wa soka.
Polisi imesema kuwa wezi hao wamejitengenezea utajiri mkubwa kabla ya baadhi yao kunaswa wakiwa na zaidi ya Dola 1.5 milioni za Marekani, walizovuna kutokana kuendesha mchezo wa kamari bila kufuata taratibu.
Kwa mujibu wa gazeti la Xinhua, Serikali ya China iliendesha msako baada ya kupata tetesi za kuwepo watu wengi wanaochezesha kamari za kutabiri washindi mbalimbali wa mechi za Kombe la Dunia.
Polisi imebainisha kuwa badhi ya wahusika walitiwa nguvuni Julai 11 mwaka huu, hata hivyo Polisi imekataa kuwataja wahusika kwa kuhofia kuvuruga upepelezi.
Msemaji wa Polisi Jimbo la Guangdong, amesema watahakikisha wanawanasa wote waliojihusisha na mitandao hiyo ya wizi wa kutumia kamari kutabiri matokeo.
“Tunafahamu kuwa wezi hawa waliendesha kamati yao kwa zaidi ya miezi minane kupitia mtandao na kujipatia wateja zaidi ya 333,000 na inadhaniwa wamevuna zaidi ya dola 1.5 bilioni,” ilisema taarifa hiyo.