Wafuasi wa Bobi Wine wakamatwa Uganda

Monday April 22 2019

 

Uganda. Wafuasi wa Mbunge na mwanamuziki, Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine wametawanywa na polisi kutokana na kukaidi agizo la kusitishwa onyesho la muziki Kampala, Arua na Lira nchini Uganda.

Polisi waliweka vizingiti eneo la ufukwe Busabala ili kuhakikisha tamasha hilo halifanyiki.

Baadhi ya watu walisombwa kwenye gari la polisi kutokana na kukaidi zuio la polisi.

Waandaaji maarufu wa matamasha ya muziki, Andrewa Mukasa  na Abbey Musinguzi walikuwa ni miongoni mwa watu walioandaa tamasha hilo la Bobi Wine, nao walikamatwa.

Awali jana Jumapili, Kamanda Msaidizi wa Polisi nchini Uganda, Assuman Mugenyi aliagiza polisi nchini humo kuzuia tamasha la mwanamuziki huyo.

Hata hivyo baada ya agizo hilo, mwanamuziki huyo ambaye pia nimwanasiasa aliandika kupitia mitandao ya kijamii akisema hatakubali kuacha haki zake zikivunjwa na kuonyesha atapambana hadi hatua ya mwisho ili kuhakikisha tamasha hilo linafanyika.

Advertisement

Advertisement