Shilole: Siwezi kumrudia Uchebe wala kumtafuta Snura

Wednesday August 12 2020

 

By Nasra Abdallah

Msanii wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Zuwena Mohamed maarufu Shilole amesema hawezi kurudiana na Uchebe aliyekuwa mume wake.

Shilole ameyasema hayo leo Jumatano Agosti 12, 2020 alipokuwa akitangaza nazi ya GSM ambayo yeye ni balozi wa bidhaa hiyo.

Alipoulizwa swali kuhusu kurudiana na aliyekuwa mume wake Uchebe, Shilole amesema "Mimi kurudiana na Uchebe ni sawa na gari bovu ulipandishe mlima, kifupi siwezi ulizeni maswali mengine”.

Shilole alitangaza kupitia ukurasa wake kwenye mitandao wa kijamii wa Instagram kwamba asitambulike kama mke wa Uchebe na hii ni baada ya kudai kuwa amekuwa akimpiga mara kwa mara.

Katika andiko hilo aliloambatanisha na picha iliyomuonesha akiwa na jeraha jichoni la kupigwa alilosema ni mume wake huyo ndio amemfanyia unyama huo.

Kadhalika zikiwa zimepita siku kadhaa tangu ampe makavu ‘live’ Snura katika mkutano wa Girl Power uliofanyika jijini Dar es Salaam na kuzua gumzo, msanii huyo amesisitiza alichofanya kwake anaona ni sawa na hana la kubadilisha ikiwemo kumuomba maamaha msanii huyo.

Advertisement

Shilole alimkemea msanii mwenzake huyo, kwa kile alichoeleza kuwa amekuwa mmoja wa watu waliofurahi kupigwa kwake na mumewe Uchebe.

Akizungumza leo Jumatano, Agosti 12,2020 na waandishi wa habari waliotaka kujua kama ameshamtafuta Snura kuliweka sawa jambo hilo,alijibu kwa kifupi kuwa 'hilo limeisha' hatarudia tena kulizungumza na wala haoni hana yankumtafuta.

Kutokana na tukio hilo baadhi ya watu walimlaumu Shilole kwa kitendo chake hicho na kueleza haikuwa sehemu sahihi kumwambia maneno yale ukizingatia ni mkutano uliokuwa na viongozi waku wa nchi na pia kufuatiliwa na Rais John Magufuli ambaye alipiga simu ukiwa unaendelea.

Kitendo hicho kilimuudhi Snura ambaye mbali ya kueleza kumdhalilisha, pia amesema amezungumza maneno ambayo hakuyasema na kuongeza kuwa kwa muda mrefu amekuwa akimchukia na alichokifanya ni mwendelezo wa chuki dhidi yake ili aonekane hafai kwenye jamii na wanawake kwa ujumla.

Shilole alipoulizwa kama ameshamtafuta msanii huyo ili kumaliza tofauti zao, Shilole amesema hawezi kwa kuwa yeye alichokifanya pale ameshamiliza na hawezi kumtafuta.

Advertisement