Sababu wachekeshaji kuitwa ‘Chale’

Thursday September 10 2020

 

By SALIM SAID SALIM

 KATIKA jamii nyingi za Waswahili na hasa Zanzibar anapotokea mtu analifanyia mzaha jambo muhimu utasikia anaambiwa acha kufanya uchale yaani mzaha. Asili ya neno chale ni jina la mchekeshaji maarufu wa michezo ya sinema wa Kiingereza, Charlie Chaplin. Tangu siku alizopata umaarufu kwa mambo ya kuchekesha Waswahili wakabuni neno chale kumueleza mtu ambaye anafanya vichekesho.

Katika nchi nyingi siku hizi watu hufanya sherehe za kukumbuka visa na mikasa ya mtu huyu pale inapowadia siku aliyozaliwa.

Bwana huyu, Charles Spencer “Charlie” Chaplin alizaliwa 1889 na kufariki duni 1977.

Kwa zaidi ya miaka 75 alishiriki katika michezo zaidi ya 50 ya sinema tangu mdogo hadi ali-pokuwa mzee na kuvutia wakubwa na wadogo duniani kote. Tokea wakati wa uhai wake na baada ya kuiaga dunia watu wamekuwa wakifurika kwenye majengo ya sinema kuangalia michezo yake. Wengine wengi wanazo majumbani mwao sahani za michezo yake. Vituo vya run-inga katika nchi nyingi havichukui muda mrefu bila ya kuonyesha mchezo wa Charlie Chaplin. Hata hapa kwetu ukipanda boti zinazosafiri kati ya Dar es Salaam na Zanzibar utaona michezo ya Charlie Chaplin inaonyeshwa.

Hii husababisha wakati wote wanaosafari kufurahi na kuwaacha hoi kwa vichekesho vya Chaplin tangu mwanzo hadi mwisho wa safari.

Charles Spencer “Charlie” alikuwa mcheza sinema mchekeshaji maarufu kuliko wenzake wote wa fani hiyo duniani.

Advertisement

Nakumbuka nilipokuwa mdogo jinsi watu walivyofurika

katika jengo la sinema kwa hata wiki nzima mchezo wa Chaplin ulipoonyeshwa.

Waswahili walivutiwa na sura iliyokuwa inachekesha na hasa alipokuwa katika kivazi alichopen-da sana cha panjama (nguo za kulalia).

Miongoni mwa michezo iliyonivutia katika miaka ya 1950 ni ule wa kuigiza ujahili wa dikteta wa Kijerumani Adolf Hitler uliotwa The Great Dictator (Dikteta Mbobezi).

Mchezo huo uliopata tuzo nyingi duniani ulifundisha mengi juu ya hatari za udikteta, iwe katika familia, jamii au nchi. Mchezo mwigine uliovutia ni Crying in the rain (Kilio wakati mvua ikin-yesha). Katika mchezo huo Chaplin alisema ukilia wakati maji ya mvua yanakuangukia watu ha-waoni machozi yako na hivyo aibu yako inafichika. Kwa ufupi, japokuwa Chaplin mara nyingi aliweka mzaha mbele kuliko mambo mengine baadhi ya nyakati alitoa ushauri wa maana na ma-funzo makubwa kwa jamii na serikali zilizojikita katika rushwa na ufisadi. Miongoni mwa mat-amshi yake muhimu katika maisha ni pale aliposema “You’ll never find a rainbow if you’re look-ing down” (Hutauona upinde wa mvua kama utaangalia chini).

Ujumbe wake muhimu katika nukuu isemayo: “Nothing is permanent in this wicked world, not even our troubles” (hakuna jambo la kudumu katika dunia hii iliyojaa maovu, hata kwa matatizo tuliyo nayo”. Alizaliwa Aprili 16, 1889 na kuwa na maisha magumu tangu akiwa mdogo. Hali ilikuwa mbaya zaidi mama yake aliyekuwa mjane alipopata matatizo ya akili na kulazwa hospitali kwa matibabu. Akiwa na miaka tisa Chaplin alipelekwa kuishi nyumba ya yatima na akiwa huko alianza kufanya kazi kama mtoto mchekeshaji katika michezo kwenye kumbi za burudani na hai-kuchukua muda alipata umaarufu. Baadaye baadhi ya michezo yake ilimpatia umaarufu mkubwa duniani na watu wengi waliopenda kuchekesha wenzao waliitwa Charlie Chaplin.

Chaplin alitengeneza, kuongoza, kuhariri na kutia muziki mwenyewe michezo yake mingi. Baadhi ya kauli zake za kukosoa mwenendo wa nchi za Magharibi zilisababisha aambiwe ni mkomunisti na hata kusababisha Shirika la Ujasusi la Marekani (FBI) lilimfukuze Marekani mwaka 1952.

Alipoelezwa kwamba ni mtu hatari alisema kama kutetea watu maskini na kulaani wasiojali mai-sha ya wanyonge ni kitu kibaya, basi alifurahi na kuona fahari kuambiwa hivyo. Hata hivyo aliru-di Marekani 1972 pale chuo maarufu cha michezo ya sinema, Academy of Motion Pictures kili-pompa tuzo maalumu ya mchango wake kwa usanii duniani.

Kuna wakati umarufu wake ulipungua, lakini baadaye alichomoza tena kwa kasi na michezo yake kupendwa.

Baadhi ya michezo yake, kuanzia alipokuwa mdogo hadi alipokuwa mkubwa iliigizwa na wachezaji sinema wengi duniani.

Chaplin alifunga ndoa na Oona, mtoto wa mwandishi wa michezo ya sinema Eugene O’Neill. Wakati walipoona, Oona alikuwa na miaka 18 wakati Chaplin ana miaka 54.

Alipoulizwa kwa nini alifunga ndoa na msichana mdogo alisema: “Raha ya maisha ni kuwa na dogodogo pembeni. Unapokuwa na msichana mdogo karibu yako basi damu yako huchangamka na kuwa kijana.” Chaplin na mkewe waliondoka Marekani na kuishi pamoja hadi 1977 alipofariki akiwa Uswisi.


Advertisement