Oka, Carpoza wasema uvumilivu ndio silaha

Muktasari:

Oka amesema kama sio sanaa basi angekuwa mwalimu wakati kapoza aliyesomea ufundi anasema alikuwa na lengo la kuwa injinia kwenye maakampuni makubwa.

SANAA ni pana na inatumika kwa maana tofauti katika jamii, japo wengi wakichukulia zaidi kama sehemu ya burudani huku ndani yake wakipata elimu ya ujumbe unaotolewa

Wachekeshaji Oscar Martin (Oka Martin) na Edward Michael 'Carpoza' wanasema kikubwa kilichowafikisha hatua ya kujulikana zaidi ni hali ya uvumilivu wa kazi yao wanayoifanya.

"Tumeanza kazi miaka mitano iliyopita, lakini matunda yake tumeanza kuona miaka miwili iliyopita, tulipita kwenye changamoto kubwa kiasi kwamba tulitaka kuacha.

"Tuliamini ipo siku tutafanikiwa kwa kuwatazama Jotti na Mpoki ambao kwa kiasi wametusaidia kuona thamani ya kazi tunayoifanya" amesema Oka.

Carpoza ameongeza hawakukata tamaa kwani wanaamini kuna deni ambalo wanatakiwa kulifanya kwaajili ya sanaa wanayoifanya.

"Tunajua sio miaka yote itatufanya tuendelee na sanaa hii maana kitakuja kizazi kingine ambacho hatuna budi kuwapisha ndio maana tunajitajidi kuwekeza"

Ameongeza kikubwa kinachoikwamisha sanaa hiyo kushindwa kuwepo kwa watu wenye taaluma katika sanaa lakini mwisho wa siku mtu mmoja hufanya kazi hata kama hana ujuzi nayo.

Oka amesema kama sio sanaa basi angekuwa mwalimu wakati kapoza aliyesomea ufundi anasema alikuwa na lengo la kuwa injinia kwenye maakampuni makubwa.