Nandy akubali kushindwa tuzo za Soundcity MVP 2020

Thursday January 16 2020

 tuzo za Soundcity MVP 2020-Mwimbaji Nandy -tuzo -Diamond- Nandy- Marioo-

 

By Rhobi Chacha

Dar es Salaam. Mwimbaji Nandy amekubali kushindwa katika tuzo za Soundcity MVP 2020, licha ya kukiri alikuwa na matarajio makubwa ya kuchukua tuzo.

Wanamuziki walioiwakilisha Tanzania katika tuzo hizo ni Diamond, Marioo, Harmonize, Ray Vanny na S2kizzy wote wametoka mikono mitupu katika vipengele vyao

Nandy alisema wasanii wengi wa Tanzania wamepata nafasi ya kuingia katika vipengele mbalimbali hiyo ni moja ya hatua nzuri japo hawajapata tuzo.

Alisema kuingia tu katika kipengele inaonyesha kazi yako imeonekana, lakini ni lazima mshindi awe mmoja wakati ukifika watashinda.

Tuzo hizo zilizotolewa Nigeria usiku wa kuamkia Jumapili Januari 12, 2020 nchini Nigeria zilijumuisha wasanii mbalimbali ya Afrika.

Advertisement