Mwijaku atoa ya moyoni kutishiwa maisha

Friday February 15 2019

 

By Nasra Abdallah,Mwananchi

Msanii wa aliyewahi kutesa katika tamthiliya ya mahusiano, Mwemba Batoni maarufu kwa jina la 'Mwijaku', amesema kamwe hatoacha kukosoa watu ambao wanaenda kinyume na masuala mbalimbali katika jamii pamoja na changamoto anazozipitia ikiwemo kutishiwa maisha.

Mwijaku ameyasema hayo leo,Ijumaa Februari 15, wakati alipokuwa kitangazwa kuwa balozi wa kampeni ya Bima ya Goose Africa na Hoteli ya Tiffany.

Amesema katoka kazi yake hiyo amekuwa akikumbana na changamoto mbalimbalinokiwemo kutaka kuuliwa na wengine kumtegea misumari kwenye gari lakini kamwe hawawezi kumrudisha nyuma kwa kuwa ni moja ya kazi ya msanii.

"Wakati katika mitandao watu hunichukulia ndivyo sivyo ninapowakosoa watu bila woga, kuna baadhi wamekuwa wakimuona ni mtu muhimu katika jamii na ndio maana leo natafutwa na watu kuniona ninafaa kkuwa balozi wao,.

" Nishaviziwa sana ikiwemo kutaka kuuliwa na wengine kunivamia nyumbani kwangu zaidi ya Mara moja,sema tu wamenikuta na mimi nipo fitina pia huenda kuripoti katika vyombo vya dola lakini nawaambia sitaacha kuwakosoa hadharani" amesema Mwijaku.

 Ametumia fursa hiyo kuwataka watu hususani vijana kutumia mitandao vizuri kwani kuna manufaa mengi na kueleza kuwa hajawahi kufikiria kuna watu wangemtafuta awe balozi wao. Naye Meneja Ufundi na Maendeleo ya Masoko wa Goose Africa Richcollins Burton, amesema kwa muda mrefu wamekuwa wakimfuatilia Mwajaku na kuona ana vitu adimu ambavyo watu wataweza kujifunza kwake.

Burton amesema kama Goose wameona ni wakati sasa wa kutoa elimu ya umuhimu wa bima kwa watanzania kupitia mitandao ya kijamii ambao wengi hawana uelewa nayo huku idadi kubwa wakiwa ni wafuasi wa mitandao hiyo.

Advertisement