Mwanamuziki Manu Dibango afariki kwa ugonjwa wa corona

Tuesday March 24 2020

Mwanamuziki Manu Dibango afariki kwa ugonjwa wa corona,Mwanamuziki mashuhuri na mpiga saxophonist wa Cameroon,Emmanuel N'Djoke Dibango ‘Manu Dibango’,

 

Paris, Ufaransa. Mwanamuziki mashuhuri na mpiga saxophonist wa Cameroon, Emmanuel N'Djoke Dibango ‘Manu Dibango’, amefariki kwa ugonjwa wa corona.

Manu Dibango amefariki leo Jumanne asubuhi akiwa nje hospitali katika jiji la Paris, Ufaransa.

Dibango mwimbaji wa muziki wa jazz mwenye miaka 86, wiki iliyopita katika ukurasa wake wa Facebook alitangaza kupatwa na ugonjwa wa virusi vya corona.

Manu Dibango anakumbukwa kwa wimbo wake mashuhuri uliotamba mwaka 1972, ulioitwa Soul Makossa.

Advertisement