Marioo ana ndoto za kutoboa tu

Friday January 24 2020

Marioo ana ndoto za kutoboa tu- NYOTA wa muziki wa Bongofleva, Marioo - mfanyabiashara mkubwa wa muziki-

 

By Rhobi Chacha

NYOTA wa muziki wa Bongofleva, Marioo amesema baada ya miaka mitano ijayo ana ndoto za kuwa mfanyabiashara mkubwa wa muziki.

Marioo aliyewashika mashabiki wa muziki huo kwa ngoma kama ‘Inatosha’, ‘Raha’ na nyingine nyingi amesema, kila msanii huwa ana ndoto zake kichwani mwake, hivyo yeye ni kutaka kuwa mfanyabiashara mkubwa wa muziki.

“Hadi sasa nashukuru baadhi ya malengo yangu niliyojipangia katika muziki, yametimia kwa asilia kadhaa, hivyo nina imani hata hii ndoto yangu niliyonayo ya kuwa hapo baadaye kuwa mfanyabiashara mkubwa wa muziki nina imani nitafanikiwa tu”alisema Marioo

Hata hivyo, Marioo ambaye ni msiri sana wa mambo yake binafsi, amesema hakuna kitu kingine anachofanya nje ya muziki kwani muziki ni maisha yake na ndiyo kila kitu kwake.

Advertisement