Mama Abdul avunja ukimya

Tuesday September 4 2018

 

MNAMKUMBUKA nyota wa zamani wa Kundi la Kaole anayetamba kwa sasa na vichekesho vya Kitimtim, Salome Nonge ‘Mama Abdul’? Mwigizaji huyo ameibuka na kutoa rai kwa wakongwe wenzake wawashike mkono chipukizi badala ya kujenga ngome ya kutengana nao wakiwazuia kuigiza nao.

“Napenda kuwaasa wenzangu hasa wakongwe tusiwabanie chipukizi katika kazi, wawasaidie hata wakipata tatizo, sisi kama kina Mzee Jongo na Mama Hambiliki wangetubania tusingefika hapa tulipo,” alisema Mama Abdul.

Mama Abdul aliyekuwa akijiuguza alisema ameamua kulisema hilo baada ya kuona wasanii wamegawanyika na baadhi kujiona ni bora kuliko wengine na pia chipukizi wakikaushiwa na wakongwe na kudai bila umoja fani haisongi mbele.

Advertisement