Kylinn maisha mapya bila bilionea Mengi

Muktasari:

  • Mengi alianza maisha yake kutoka familia ya umaskini na kuja kuwa mmoja kati ya matajiri wakubwa barani Afrika akiwa na utajiri wenye thamani ya zaidi ya Dola 400 milioni

Kwa kipindi cha wiki mbili hivi zilizopita kule Tanzania, stori kubwa ilihusu kifo chake bilionea mgusa nafasi za watu, Dk Reginald Mengi aliyefariki dunia kule Dubai akiwa na umri wa miaka 77,  huku nyuma akiiacha familia yake na watu wanaomtegemea kwenye jamii.
Mengi alikuwa sio tu tajiri wa mali, pia tajiri wa roho. Alikuwa ni mtu wa hisani na mwenye kupenda kutoa. 
Kifo chake kiliwagusa wengi akiwemo Rais John Magufuli aliyemwaga machozi kwenye misa ya wafu. 
Watu wengi wakiwemo wanaoishi na ulemavu walimtegemea kwa misaada na ni miongoni mwa wale waliohuzunishwa zaidi na kifo chake. 
Mengi alianza maisha yake kutoka familia ya umaskini na kuja kuwa mmoja kati ya matajiri wakubwa barani Afrika akiwa na utajiri wenye thamani ya zaidi ya Dola 400 milioni.
Pia alikuwa na maisha yake ya kibinfasi. Kamwacha nyuma mke wake mchanga, Jacqueline Ntuyabaliwe MengiKylnn’ mwenye miaka 39 aliyemzalia pacha ambao bado ni makinda.
Kwa walioanza kufuatilia muziki tangu miaka ya nyuma takriban 15 zilizopita, basi Kylnn ni jina la kukumbukwa kwa urahisi.
Enzi hizo alikuwa mmoja kati ya wanamuziki mastaa waliokuwa wakitisha kwenye muziki wa kisasa. 
Kylnn aliyewahi pia kuwa Miss Tanzania, alijipatia umaarufu mkubwa kwa kuachia hiti kadhaa kama vile ‘Crazy Over You’, ‘Chochote Utapata’, ‘Nalia kwa furaha’, ‘Nipe Mkono’.
Kylnn alistaafu muziki baada ya kukutana na Mengi na kuolewa naye. Amedumu kwenye ndoa naye kwa zaidi ya miaka saba hadi kifo chake. Hata hivyo, baada ya kifo chake Mengi, stori kibao zimekuwa za kumhusu Kylnn. 

Hii ni ijapokuwa wakati Mengi anakutana na Kyln tayari alikuwa staa. Wakikutana nyota ya Kylnn ilikuwa inang’aa. Kylnn alikuwa anafanya muziki na biashara.