Kiki : Dulla Makabila ajipodoa kama mwanamke kisa 'Ningekuwa Demu Ingekuwaje’

Tuesday February 11 2020

Kiki : Dulla Makabila ajipodoa kama mwanamke kisa 'Ningekuwa Demu Ingekuwaje’

 

By Rhobi Chacha

Dar es Salaam.Imezoeleka kwa baadhi ya wasanii wa bongofleva kufanya kiki kabla hawajatoa nyimbo zao. Wapo wanaofanya kiki na kupokelewa vema na wengine kiki zao zinabuma na kuishia kutukanwa mitandaoni.

Hii imetokea siku mbili zilizopita baada ya msanii wa singeli Dulla Makabila kutuma picha katika akaunti yake ya instagram inayomuonyesha akiwa amejiremba  na kuwa na muonekano wa mwanamke.

Picha hiyo inayomuonyesha Makabila akiwa amejipodoa huku kichwani akiwa amevaa nywele bandia (wigi), jambo lililozua utata kwa mashabiki wake waliomtolea maneno kali mtandaoni.

Hata hivyo, baada ya picha hiyo jana, Dulla aliweka picha hiyo tena na kuandika ujumbe 'Ningekuwa Demu Ingekuwaje?' na maelezo yanayotambulisha kuwa ilikuwa ni wimbo.

Pamoja na kufanya hivyo bado mashabiki wake wanaendelea kumponda kwa kitendo hicho cha kujigeuza mwanamke.

Kiki ya aina hii ya kujifafanisha na mwanamke ilishawahi kufanywa na msanii wa bongofleva Dogo Janja katika wimbo wa Wayu wayu ambapo alijipodoa na kuvaa nywele bandia na kuambulia matusi mitandaoni.

Advertisement

 

 

 

 

 

 

 

Advertisement