Dully, Maua Sama kuna jambo

Friday October 16 2020
dullyy picc

Ukipitia akaunti ya Instagram ya Mr. Misifa Dully Sykes utagundua watu wengi wanamfollow, lakini yeye anamfollow mtu mmoja tu ambaye ni staa wa ngoma ya Iokote, Maua Sama.

Kwa nini Maua Sama? Jarida la Jiachie lilimtafuta Dully Sykes na kumbana aeleze sababu kwanini hali imekuwa hivi kati yake na Maua Sama.

“Umeona watu wengi wananifollow, kwa sababu mimi ni msanii wanayenikubali. Na mimi kwa sasa msanii ninayemkubali zaidi ni Maua Sama ndo maana nimemfollow,” ameeleza Dully.

Aidha, hivi karibuni Dully alitangaza kuwa anaanzisha lebo yake itakayoitwa Misifaz ambayo itakuwa inafanya shughuli za kuwasimamia wasanii. Sasa kwa sababu bado lebo hiyo haina msanii yeyote, Dully aliulizwa kwamba hii ya kumfollow Maua Sama peke yake haiwezi kuwa dalili kwamba anajiandaa kumsajili msanii huyo kwenye lebo yake? Dully amejibu;

“Lebo itaanza kazi rasmi mwezi Desemba, kwahiyo kwa kipindi hiki tuwe wapole tu. Ingawa ninachoweza kusema ni kwamba yote yanawezekana.” ameeleza Dully.

Oktoba mosi Dully Sykes aliachia wimbo unaoitwa Naanzaje ambao ndani amemshirikisha Maua Sama.

Advertisement
Advertisement